Balile aipongeza MSD kufanya kazi na viwanda vya ndani
![]() |
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, akitoa neno la shukrani kwa waandaaji wa mkutano, Bohari ya Dawa (MSD) |
Na Frank Balile
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus
Balile, amewapongeza Bohari ya Dawa (MSD), kwa jitihada zao za kuhakikisha
wanafanya kazi na viwanda vya ndani.
Ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha
maafisa wa MSD na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kilichofanyika
Septemba 27,2023 jijini Dar es Salaam. Balile alisema kuwa, ni jambo zuri sana
la kufanya kazi na viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa za afya, badala ya
kuagiza nje ya nchi.
"Niwapongeza sana kwa uamuzi wenu wa kuvitumia viwanda vya
ndani vinavyozalisha bidhaa za afya, inasaidia kupunguza gharama na kuinua
uchumi wa nchi," alisema. Balile amesema tangu MSD wafanye mabadiliko, imeonesha
muelekeo mzuri sana katika kujali afya za wananchi kwa kuhakikisha dawa na
vitendea kazi vinapatikana.
Mwenyekiti huyo wa TEF, amempongeza Msajili wa
Hazina, Nehemia Mchechu na timu yake kwa kuanzisha utaratibu wa taasisi zilizo
chini yake zinakutana na wahariri na waandishi wa habari kueleza kazi zao.
"Nampongeza Msajili wa Hazina, ndugu yetu Mchechu kwa kuliona hili, itasaidia
sana wananchi kuzifahamu vizuri taasisi na majukumu yake," alisema.
Alisema
kuwa, thamani ya taaluma ya habari inatakiwa kuheshimiwa, ikiwa pamoja na kupata
taarifa sahihi kwa wakati sahihi bila vipingamizi.
Amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai, kwa mipango yake mizuri ya kuhakikisha taasisi hiyo inakuwa msaada mkubwa kwa watanzania katika suala la afya.
![]() |
Mhariri Joseph Kulangwa atoa ushauri kwa maafisa wa MSD |
![]() |
Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano Bohari ya Dawa (MSD), Eti Kusiluka, Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, Hassan Ally, Mkurugenzi Mkuu, Mavere Tukai, Mkuu wa Kitengo cha Habafri na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Anthony Mkuti na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, wakishiriki kikao kazi. |
No comments