Waziri Mchengerwa, wabunge washuhudia wanyama wakivuka Mto Mara
WAZIRI wa Maliasi na Utalii, Mohamed Mchengerwa, baadhi ya wabunge na wageni kutoka mataifa mbalimbali wameshuhudia tukio Kubwa duniani la wanyama kuvuka Mto Mara.
Tukio hilo maarufu duniani linajulikana kwa jina la Serengeti Grand Migration likiwa la kwanza lililofanyika kwenye eneo la Kogatende, Serengeti, huku wageni mbalimbali kutoka mataifa mengi wakiungana na viongozi hao kushuhudia kwa zaidi ya saa mbili.
Wanyama aina ya nyumbu ambao walikuwa wengi walikuwa wakisindikizwa na pundamilia kuvuka na kupitia majaribu mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mamba kwenye Mto Mara.
Viongozi alioongozana nao Waziri wa Utalii ni Naibu wake, Mary Masanja, Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Benedict Wakulyamba, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Timotheo Mnzava, ambaye aliongoza baadhi ya wajumbe wa Kamati hizo kushuhudia tukio hilo la kihistoria na kubaki wakishangazwa na maajabu hayo.
“Ndiyo tumeanza kutekeleza mikakati ya kuutangaza utalii wetu, tukio hili ni la kihistoria na huwezi kulikuta popote duniani, ujio wetu hapa ni kukipa heshima na kulitangaza zaidi duniani,” amesema Waziri Mchengerwa.
“Tumejionea maajabu leo na tunaipongeza Serikali na wahifadhi wetu kwa kuwalinda wanyama hawa mpaka leo, tumejionea tukio hili la aina yake,” amesema Mwen kamati ya Bunge ya ASridha, Maliasi na Utalii, Mnzava.
No comments