WAZIRI MABULA ATAHADHARISHA WANAOTUMIA WIZARA KAMA REJEA KUFANYA UHALIFU
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mgogoro wa kiwanja kilichopo eneo la Viwanda
Mbezi jijini Dar es Salaam, Agosti 14, 2023.
Na Mwandishi wetu, WANMM
WAZIRI wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa tahadhari kwa
wale wanaotumia wizara yake kama rejea kufanya uhalifu na kujipatia mali au
fedha isivyo halali. Waziri Mabula amesema mtu yoyote akihisi kuna udanganyifu
ndani na nje ya Wizara ya Ardhi atoe taarifa mapema ili kukomesha uhalifu huo.
Dkt Mabula alitoa kauli hiyo leo tarehe 14 Agosti 2023 mbele ya waandishi wa
habari jijini Dodoma kufuatia wizara yake kupokea malalamiko ya muda mrefu
kutoka kwa familia ya marehemu Zuberi Mzee Mwinyimvua inayodai kwamba wizara
yake haitaki kuondoa Hati ya kuwekesha (Notice of Deposit) iliyosajiliwa katika
daftari la Msajili wa Hati kuhusu kiwanja Na 895 kilichopo eneo la viwanda mbezi
mkoani Dar es Salaam iliyiosajiliwa ili kutoa kinga ya uwekezaji.
Kwa mujibu wa
Dkt Mabula, kiwanja hicho kinamilikiwa na Mwinyimvua ambaye kwa sasa ni
marehemu. Akifafanua zaidi, alisema awali mmiliki wa kiwanja hicho aliingia
mkataba wa uwekezaji na Velence Simon Matunda na Badi Nkya wanaotambulika kama
wawekezaji.
Uwekezaji huo ulikuwa ni kujenga maduka 40 ambapo kati ya hayo
maduka 33 yangesimamiwa na wawekezaji kwa kipindi cha miaka 15 na baada ya hapo
wangekabidhi maduka hayo 15 kwa mmiliki ambapo katika kipindi hicho cha miaka 15
wawekezaji wangekusanya kodi ya pango.
Kwa mujibu wa mkataba, mmiliki alipewa
kiasi cha shilingi 90,000,000 kwa ajili ya kulipa madeni ikiwemo kodi ya pango
la ardhi la kiwanja hicho. Waziri Mabula alisema suala la mgogoro huo limekuwa
likishughulikiwa kiutawala kupitia wizara ya ardhi kwa zaidi ya miaka 8
kuhakikisha kwamba wawekezaji wanalipwa fedha hizo kama mahakama ilivyoamuru ili
hatimaye msajili wa hati aondoe hati ya kuwekesha katika daftari la msajili na
kukabidhi hati husika.
Kwa mujibu wa waziri Mabula, mpaka sasa suluhu ya mgogoro
huo haijapatiakana kutokana na pande mbili za mgogogoro yaani msimamizi wa
mirathi na wawekezaji kutotekeleza yale waliyokubaliana hususan upande wa
uwekezaji.
Kimsingi mgogoro huo unatokana na ukiukwaji wa makubaliano baina ya
mmilikina wawekezaji ambapo pia mahakama ilishatoa maamuzi. Wizara inatimiza
wajibu wake kiutawala katika kutatua mgogoro pamoja na kuwa suala hilo linahusu
mkataba wa uwekezaji na siyo umiliki wa ardhi.
Waziri Mabula alisema kwa kuwa
mgogorio huo ni wa muda mrefu na wahusika wanaihusisha wizara ambayo si sehemu
ya makubaliano na hivyo kuharibu taswira ya wizara ameelekeza pande zote za
mgogoro kuheshimu na kutekeleza hukumu ya mahakama sambamba na pande hizo
kutekeleza yale wanayokubaliana katika vikao vya usuluhusshi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na mgogoro wa kiwanja kilichopo eneo la Viwanda
Mbezi jijini Dar es Salaam Agosti 14, 2023.
Pia, amemuelekeza katibu Mkuu wizara
ya ardhi kushirikiana na vyombo vya dola kuingilia kati suala hilo kwa kuwa una
sura ya kijinai na utapeli ndani yake.
No comments