Header Ads

ad

Breaking News

Watumishi wawili Kibaha watimuliwa kazi kwa ubadhilifu

Na Omary Mngindo, Mlandizi

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha (Kibaha Vijijini) Mkoa wa Pwani, imeazimia imewafukuza kazi watumishi wawili kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za halmashauri hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Erasto Makala, mbele ya Baraza la Madiwani, amesema watumishi hao wamekiuka kanuni ya 42 ya mwaka 2022, kwa kutumia vibaya madaraka yao hali iliyoisababishia hasara halmashauri hiyo.

Amesema mmoja amefukuzwa baada ya kutumia marejesho ya vikundi kiasi cha shilingi milioni 28.2 na mwingine kupoteza vitabu 20 na pesa taslimu shilingi milioni 3.5.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Butamo Ndalahwa ameliambia baraza hilo kwamba, wamepokea maelekezo hayo, na kwamba watahakikisha wanayafanyia kazi kwa kuwachukulia hatua watumishi wanaokwenda kinyume cha taratibu za kazi.

"Tumepokea maagizo, nakuahidi Mwenyekiti na Baraza lako kwamba, tutalifanyia kazi suala hili, kwani haliwezi kufumbiwa macho," amesema Ndalahwa.

Baraza hilo limemthibitisha Shomari Minshehe kuwa Makamu Mwenyekiti, akipokea mikoba ya Josephine Gunda aliyemaliza kipindi chake cha mwaka mmoja wa utumishi wa nafasi hiyo.

Minshehe alisema, "Nimesikia kuna baadhi ya watumishi wana hofu na mimi kuhusiana na nafasi hii niliyoipata, sina tatizo na mtumishi anayetimiza wajibu wake ipasavyo," amesema Minshehe.

Akitoa shukrani kwa madiwani, mkurugenzi na watumishi wote, Gunda amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja amepata ushirikiano mkubwa uliomwezesha kuitumikia vizuri nafasi ya makamu mwenyekiti.



No comments