TTCL yajipanga kulifikisha Taifa katika uchumi wa kidigitali
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mhandisi Peter Ulanga |
Akizungumza na wahariri leo tarehe 24 Agosti 2023, jijini Dar es Salaam kuhusu mwelekeo wa shirika hilo katika miaka mitano ijayo amesema, ni kujenga ubunifu wa hali ya juu katika safari ya kulipeleka taifa kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda.
“Tulikuwepo miaka 120 iliyopita, tutakuwepo miaka 120 ijayo. Tumebeba jukumu zito la kuifikisha nchi katika Uchumi wa Kidigitali.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile |
"Mkaguzi Mkuu (CAG), huangalia kasoro tu kwenye shirika, hivyo hata kama mna mnamafanikio 100 na kasoro 10, yeye ataandika kasoro hizo tu maana ndio kazi yake, hivyo unaweza kudhani shirika lote lina dosari jambo ambalo si kweli- Mkurugenzi Mkuu TTCL, Mhandisi Peter Ulanga akizungumza na wahariri Agosti 24, 2023 jijini Dar es Salaam.
“TTCL tunajiangalia kwa upana zaidi, si kama shirika la kutoa huduma ndani ya nchi tu, bali shirika kubwa linaloweza kutoa huduma nje ya mipaka ya nchi, ndani ya mwaka huu tutaanza kutoa huduma yetu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), amesema Ulanga.
Amesema, anatamani taifa lifike katika hatua ya kutotembea na pesa (cashless) na kwamba, shirika hilo ni miongoni mwa wadau katika kufikia hatua hiyo.
“Tunataka ifike mahali matumizi ya cash yasiwepo. Tutawahimiza na wadau wengine tufike kwenye cashless,” amesema.
No comments