Header Ads

ad

Breaking News

SIMBA YAANZA KUHESABU POINTI, YAIPASUA MTIBWA SUGAR 4-2

 


MAB INGWA wa Ngao ya Jamii, Simba SC Agosti 17, imeifunga Mtibwa Sugar mabao 4-2, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.

Mtibwa Sugar wakiwa nyumbani walikubali kufungwa bao la kwanza dakika ya tano lililowekwa kimiani na Jean Baleke dakika ya tano, huku Willy Onana akiongeza b ao la pili dakika ya tisa.

Hata hivyo, Matheo Anthony aliipatia Mtibwa Sugar bao la kwanza dakika ya 20 na kuisawazishia timu yake bao la pili dakika ya 22.

Simba, walibadilika na kuanza kulisakama lango la wapinzani wao, dakika ya 45, kiungo mpya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Fabfrice Ngoma aliiandikia bao la tatu.

Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama aliwamaliza nguvu Mtibwa Sugar, baada ya kufunga bao la nne dakika ya 81, hivyo Wekundu wa Msimbazi wakafanikiwa kuondoka na pointi zote tatu katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC.



No comments