Header Ads

ad

Breaking News

Shule ya Mwalimu Nyerere yapokea wanafunzi 2019

Na Omary Mngindo, Kibaha 

SHULE ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha kwa Mfipa Mkoa wa Pwani, hadi Julai 31,2023 imeshapokea viongozi 2019 ambao wanatumia shule hiyo kijiendeleza zaidi kielimu. 

 Hayo yamebainishwa na Mkuu wa shule hiyo,Profesa Marcellina Chijoriga, akizungumza na Waandishi wa habari baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda kufungua mafunzo ya uongozi kwa wanafunzi 52 walioanza mafunzo shuleni hapo. 

 Mafunzo hayo ya 19 tangu kufunguliwa kwa shule hiyo Februari 23,2022 na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, imepokea jumla ya taasisi 40 ambazo zimefika kwa ajili ya mafunzo tofauti yanayolenga kuwanoa watumishi wa sekta mbalimbali.

 "Hadi Julai 31,2023 jumla ya taasisi 40 zimeitumia shule yetu kuwaongezea ujuzi wafanyakazi wao, watumishi wapatao 2019 kutoka mashirika na taasisi hizo zimefika shuleni hapa kuwaongezea ujuzi wafanyakazi wao," alisema Profesa Chijoriga. 

 Aliongeza kuwa, shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyojengwa kwa ushirikiano wa vyama tawala vya nchi sita za Kusini mwa Afrika mwaka 1960 hadi 1990, huku akikitaja kingine cha saba ni CPC pamoja na Serikali ya China ndiyo waliofadhili ujenzi huo. 

 "Tangu shule ifunguliwe Februari 23,2022 hadi sasa imeendesha kozi 19, saba zilitolewa na vyama rafiki, 12 Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sekta binafs,jumla ya wahitimu 2019 wameshiriki kozi hizo," alisema Mkuu huyo. 

 Aliishukuru CCM chini ya Mwenyekiti wake Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuiangalia shule hiyo inayotoa huduma za mafunzo kupitia mashirika, taasisi na chama hicho. "Tuna kumbi za mikutano kwa idadi ya washiriki mbalimbali, tunaziomba taasisi kuzitumia kwa warsha na mafunzo mbalimbali," alisema mkuu huyo.

No comments