POSTAMASTA AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA SHIRIKA LA POSTA
POSTAMASTA Mkuu, Daniel Mbodo amewashauri Watanzania kutumia Shirika la Posta kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi kwa kwani ni salama zaidi.
Mbodo ameyasema hayo Agosti 14,2023, wakati akizungumza na wahariri kwenye semina iliyofanyika jijini Dar es Salaam, iliyolenga kueleza kazi, changamoto, mafanikio na fursa zilizomo kwenye shirika hilo.
“Posta kuna fursa kwa wajasiriamali, sajili biashara yako bure kwenye duka la mtandaoni la posta (www.stamps.tz.post), kisha unaweza kuuza bidhaa yako ndani na nje ya nchi kwa urahisi kabisa,” amesema Mbodo.
Amesema shirika hilo limeweka malengo ya kufuta historia ya shirika kupata hasara, baada ya mwaka jana kumepata faida ya shilingi bilioni 3.37, ambapo kwasasa wameweka malengo kufikia mwaka 2024/25 kuzalisha faida ya shilingi bilioni 21.
“Katika maisha yote ya posta, haijawahi kusaidiuwa na serikali Kama kipindi hiki cha Rais Samia Suluhu Hassan, hakika tumepiga hatua kubwa na kupewa heshima kubwa kimataifa,” amesema Mbodo.
No comments