Header Ads

ad

Breaking News

MKUU WA MKOA DAR AKAGUA SOKO LA SAMAKI FERRY

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila Agosti 15, 2023 amekagua soko la Kimataifa la Samaki la Ferry na baadaye kuzun gumza na wafanyabishara wa samaki katika Soko la Ferry lililo[po wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

Chalamila alisema Rais SamiaSuluhu Hassan ana nia njema na wafanyabishara wa soko hilo na kuwataka kuwa, mlinzi wa mwenzake ili idadi ya wafanyabishara iliyopo sasa ya zaidi 3,000 isiongezeke hadi Serikali itakapofanya maboresho ya Soko.

Amesema amebaini ukosefu wa uaminifu miongoni mwa wafanyabishara kupitia kiwango cha mapato ambacho kinatakiwa kipatikane, ubovu wa miundombinu na sheria ambazo si shirikishi hivyo, ni wakati muafaka wa kuanza kupangana.

Mkuu wa Mkoa amemtaka meneja wa soko hilo kuwa na ubunifu zaidi katika kuongeza mapato na kwamba, sheria zilizoko ziwe shirikisha kwa wafanyabiashara wenyewe.

Chalamila ameagiza kupunguza matumizi ya mkaa katika soko hilo ambayo huzalisha moshi, huku akiwataka kuanza matumizi ya gesi.

Mkuu wa Wilaya ya IIala, Edward mpogolo, kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, amesema pamoja juhudi kubwa inayofanywa na Wilaya hiyo, ziko changamoto kadhaa katika soko hilo ikiwemo migogoro kati ya kanda moja na nyingine.

Ametaja changamoto nyingine ni ukosefu wa friji la kuifadhia samaki kwa baadhi ya maeneo, wafanyabishara ni zaidi ya 3,000, na kuwepo kwa mchanga kando ya ferry hiyo.

Amesema awali meli za samaki zilikuwa zinatia nanga na siku hizi haiwezekani hivyo, ujio wa Mkuu wa Mkoa imekuwa faraja kubwa na wako tayari kumsikiliza na kupokea maagizo na maelekezo yake kwa masilahi ya wafanyabishara katika soko hilo.

No comments