Header Ads

ad

Breaking News

Mbunge Koka kuzindua jogging ya Mwambisi Jumamosi

Na Omary Mngindo, Kibaha

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mji Mkoa wa Pwani, Silvestry Koka, Agosti 26,2023 atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jogging ya Mwambisi yenye makao yake makuu Kata ya Kongowe mjini hapa.

Klabu hiyo inayoundwa na vijana wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), katika kata hiyo, itazinduliwa na mbunge huyo ikiwa ni mkakati wake wa kuhakikisha vijana na wakazi wa rika mbalimbali wanashiriki michezo.

Akizungumza na Faharineews ofisini kwake, Katibu Msaidizi wa Mbunge Koka, Saidi Mbecha amesema kuwa, mbunge huyo atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo utaofanyika kwenye Uwanja wa mpira wa Tafoli uliopo Mtaa wa Mwambisi katani hapo.

"Agosti 26,2023 Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mji mkoani Pwani, Silvestry Koka, atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa klabu ya Jogging ya Mwambisi iliyopo Mtaa wa Mwambisi Kata ya Kongowe, huu ni mwendelezo wa mbunge katika medani hii ya michezo," amesema Mbecha.

Mwenyekiti waKlabu ya Jogging ya Mwambisi, Selemani Mohamed amesema maandalizi kuelekea uzinduzi huo yamekamilika, huku akiwaomba wanamichezo na wakazi mtaa na Kata hiyo kujitokeza kwa wingi.

"Jumamosi ya Agosti 26,2023 tutandika historia ndani ya mtaa wetu wa Mwambisi, utafanyika uzinduzi wa klabu yetu ya jogging, mgeni rasmi mbunge wetu Koka, niwaombe wakazi wote tujitokeze kwa wingi," amesema Selemani.

Naye, Katibu wa tawi na klabu hiyo, Victoria Aman amesema wanaungana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, kushiriki kikamilifu kwenye michezo, huku akitoa wito kwa vijana kuungana kushiriki michezo inayosaidia kuboresha afya, mahusiano na ajira.

"Kwa niaba ya wana Jogging wa Mwambisi tunamshukuru mbunge wetu kwa jinsi anavyojikita katika nyanja zote ikiwemo michezo na burudani, Agosti 26,2023 atakuwa mgeni rasmi uzinduzi wa jogging yetu katika Uwanja wa Tafoli," amesema Amani.

Selina Nchimbi amesema kuwa, wamejipanga kikamilifu kwa michezo aina yote na kwamba, siku hiyo kutakuwa na burudani ya aina yake kwenye uwanja huo, huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi.

No comments