Header Ads

ad

Breaking News

JKCI KUTOA MATIBABU YA MOYO MKOANI KILIMANJARO

Na Mwandishi Wetu 

 WATAALAM wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi iliyopo mkoani Kilimanjaro watatoa huduma za tiba mkoba zinazojulikana kwa jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Program kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani.

 Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia Agosti 21, 2023 hadi Agosti 25,2023 saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 jioni, katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi.

 Kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

 Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam. 

 “Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.”

No comments