Header Ads

ad

Breaking News

Dkt.Mpango awanoa wakuu wa mikoa, makatibu tawala

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango

Na Omary Mngindo, Kibaha

MAKAMU wa Rais Dkt. Isdory Mpango, amewataka Wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuendeleza ushirkiano na viongozi wa taasisi mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao.

Dkt. Mpango alitoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku sita yanayohudhuriwa na viongozi hao, yakifanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani, ambapo mahusiano kati yao na taasisi yana muhimu mkubwa.

Aidha, Makamu wa Rais amezungumzia migongano kati ya Wakuu wa mikoa na makatibu tawala, inayohusiana na masuala ya usimamizi wa fedha kwenye maeneo yao, hatua inayokwenda kinyume cha taratibu, huku akiwataka kurekebisha changamoto hizo.

"Kuna mifano ya baadhi ya matukio ya kutozingatiwa kwa mipaka ya kiutendaji kati ya mkuu wa mkoa na katibu tawala kuhusu masuala ya fedha, hii ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu, katibu tawala ndiye msimamizi mkuu wa masuala hayo," amesema Makamu wa Rais.

Amewapongeza kwa kutekeleza majukumu yao, kwa kumpa heshima Rais Samia Suluhu Hassan, "Nawapongeza kwa kusimamia kazi mlizopewa, lakini kuna kuvuja kwa siri za serikali, ambapo utazikuta kwenye mitandao ya kijamii, muwe na usimamizi mzuri wa masuala ya msingi ya ulinzi na usalama," amesema Dkt. Mpango.

Taarifa ya Waziri wa Utumishi ikisomwa na Naibu Waziri, Ridhiwani Kikwete imezungumzia umuhimu wa mafunzo hayo, huku ikieleza kwamba, wakuu hao ni kiungo muhimu katika utawala bora kwa nchi.

"Kwenye Ibara ya 61, ibara ndogo ya 4 katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaeleza kuwa, Wakuu wa mikoa na makatibu tawala wana wajibu wa kusimamia ipasavyo shughuli za kiserikali kwenye maeneo yao," imeeleza sehemu ya taatifa hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seriali za Mitaa (TAMISENI), Angellah Kairuki, kupitia taarifa yake imeeleza kwamba, mafunzo hayo ni mwendelezo kwa viongozi wa serikali kwa ngazi mbalimbali.

"Serikali inayoongozwa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na utoaji wa mfunzo kwa viongozi ngazi mbalimbali unayolenga kuwajengea uwezo katika utendaji wenu," amesema.







No comments