CHONGOLO AWATAKA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALI KUONGEZA UBUNIFU
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amewaagiza maafisa mawasiliano serikalini kuongeza ubunifu katika kuhakikisha wanayaelewa maeneo wanayoyafanyia kazi.
Mbali na hilo, amewataka pia kuitumia ipasavyo mitandao ya kijamii ili kuhabarisha umma kuhusu wapi serikali ilipotoka, ilipo na inapoelekea.
Chongolo ametoa wito huo Mjini Karatu Mkoani Arusha katika kikao kazi cha mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa Mkoa wa Arusha.
Amesema viongozi wengi wamekuwa wepesi kukimbilia vyombo vya habari kuelezea kero za maeneo wanayoyaongoza, lakini serikali inapotatua kero hizo wamekuwa wazito kutumia vyombo vya habari au vitengo vya habari na mawasiliano serikalini kuelezea namna serikali ilivyotatua kero hiyo ili watanzania waelewe.
Mtendaji huyo mkuu wa CCM, amesema licha ya serikali kupelekeka fedha za miradi kwa wananchi, bado changamoto imekuwa ni kwa baadhi ya maeneo kutovitumia vitengo vya habari na mawasiliano serikalini kutangaza mafanikio hayo.
No comments