Waziri Aweso amemteua Bi .Nelly Msuya kuwa Kaimu Mkurugenzi Mwauwasa
Bi.Nelly Msuya
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amemteua Bi. Nelly Msuya kuwa, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).
Mbali na uteuzi huo, Waziri Aweso ameteua wataalamu kutoka Sekta ya Maji
watakaoshughulikia changamoto ya maji kwa wakazi wa Jiji la Mwanzana kusimamia
kukamilika kwa mradi wa kuongeza maji katika mfumo wa usambazaji majisafi jijini
humo.
Wataalam hao wataongozwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maji makao makuu
ambao ni Mhandisi Mkama Bwire, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji, Wakala wa Maji na
Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na Mhandisi Charles Mafie, Mkurugenzi
Msaidizi Uendeshaji na Matengenezo, Wizara ya Maji.
No comments