Header Ads

ad

Breaking News

WATANI WA JADI KUUMANA JULAI 5 UWANJA WA TAIFA

Mwandishi Wetu

WATANI wa jadi, Simba na Yanga, watashuka Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam julai 5, 2018 kucheza mechi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki (Kombe la Kagame), ikiwa ni mechi ya Kundi C ya Michuano inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
 
Katibu wa Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye amezitaja timu nyingine za Kundi C ni Dakadaha ya Somalia na Saint George ya Ethiopia.
 
Musonye alisema kwamba Kundi A linaundwa na timu za Azam FC, KCCA ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC wa Sudan Kusini, wakati Kundi B linaundwa na timu za Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti.

Katibu huyo hakusita kuishukuru Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa michuano hiyo, kwani anakumbuka jinsi ilivyokuwa ikifuatiliwa miaka ya nyuma hasa kwa kujaza mashabiki wa soka uwanjani.
 
Michuano hiyo itapigwa katika viwanja vya Taifa na Azam Complex, ambapo kwa mwaka huu  Rais Paul Kagame wa Rwanda amedhamini mashindano hayo kwa zaidi ya miongo miwili sasa.
 
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando amesema watatumia mashindano hayo kuzindua kituo chao cha Redio cha Uhai FM, huku akiweka wazi kwamba, mashindano hayo yatafanikiwa.

No comments