Header Ads

ad

Breaking News

Raia wa Afrika Kusini washangazwa na kwaya ya 'utupu' shuleni


Waziri wa elimu ya msingi Angie Motshekga alisema kuwa mashindano hayo ni ya unyanyasaji
 Densi ya 'utupu' ya kundi moja la kwaya ya shule nchini Afrika Kusini imevutia hisia za uchunguzi kufanywa kutoka kwa waziri wa elimu nchini humo.


Angie Motshekga alisema kuwa alisikitika baada ya kuona kanda ya video ya wasichana hao wa Xhosa wakicheza densi yao huku wakiwa wamevalia nguo inayojulikana kama "inkciyo".

Waziri huyo wa elimu ya msingi alisema kuwa ni ukosefu wa heshima kwenda kinyume na maadili ya tamaduni za taifa hilo.

Hatahivyo kiongozi wa kwaya hiyo ametetea hatua yao akisema kuwa ni fahari kubwa.
Kulingana na mtandao wa Daily Dispatch nchini humo, mwalimu huyo ambaye hakutajwa alisema: Ni fahari kubwa kucheza densi ya kitamaduni ya Xhosa. Tunafurahia 'inkciyo'. Ni fahari kubwa kwa wanawake na wasichana wa Xhosa.

Kabila la Xhsoa ndilo kabila la pili kwa ukubwa nchini Afrika Kusini.
Picha za densi hiyo katika mashindano huko Mthatha, mashariki mwa Cape ,zilionekana mapema wiki hii, zikiwaonyesha wasichana hao wakicheza densi huku vifua vyao na makalio yakiwa wazi.
Kanda hiyo ya video ilipigwa wakati wa sehemu ya tamaduni ya Xhosa kulingana na mtandao wa Afrika Kusini wa Timeslive.

Swala hilo limewasilishwa katika idara ya kitaifa ya bi Motshekga.

"Ni makosa makubwa sana kwa baadhi ya walimu ambao wanafaa kujua zaidi ya kuwanyanyasa wasichana wadogo'' , chombo cha habari cha AFP kilimnukuu akisema katika taarifa.

"Hakuna makosa kupenda tamaduni na urathi wako , lakini hakukuwa na haja yoyote kucheza densi wakiwa utupu''.

"Tabia hiyo mbaya inaenda kinyume na maadili ya tamaduni zetu''.

No comments