NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI,DARASA LA NNE
BARAZA la Mitihani Tanzania
(NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na
kidato cha pili iliyofanyika Novemba mwaka jana, huku idadi kubwa ya
wanafunzi wakifaulu vizuri katika mitihani hiyo.
Akitangaza matokeo hayo leo
Jumatatu, Januari 8, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde
amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne
wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.
Amesema wanafunzi hao
wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi
72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni
ufaulu usioridhisha.
Kuhusu matokea ya upimaji wa
kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na
asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa kufanya mtihani huo
wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
Dk Msonde alisema wanafunzi wa
kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama
za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
No comments