Moses Machali amnadi Damas Ndumbaro jimboni Songea
Moses Machali akimnadi Dkt Damas Ndumbaro |
Wakati kampeni za kuelekea uchaguzi
mdogo wa jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma zikiendelea katika kata
mbalimbali za manisipaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya kumpata
mbunge wa jimbo hilo ambaye chama cha mapinduzi kimemteua Dkt Damas
Ndumbaro kupeperusha bendera ya chama hicho waliokuwa viongozi na
wanachama wa vyama vya upinzani nchini wamezidi kujitokeza kwenye
kampeni hizo na kutangaza kuachana na vyama vyao vya awali.
Miongoni mwa viongozi hao wa vyama vya
upinzani ni pamoja na waliokuwa wajumbe watatu wa serikali ya mtaa wa
Majengo mjini Songea kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo
ambao walitangaza uamuzi huo wa kukihama chao hicho na kujiunga na chama
cha Mapinduzi baada ya hotuba ya siku mbili mfululizo kwenye kampeni
hizo za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha
mapinduzi iliyotolewa na aliyewahi kuwa mwanachama wa chama na kingozi
pia cha Demokrasia na maendeleo Moses Machali.
Katika hotuba yake ya kumnhadi mgombea
huyo Machali alieleza sifa alizo nazo mgombea Dkt Damas Ndumbaro ambazo
alizifahamu muda mrefu tangu akiwa kwenye kambi ya upinzani ambazo
alisema hazina mashaka yoyote ya kumfanya asichaguliwe kuwa mwakilishi
wa wananchi wa jimbo hilo na kuwataka wananchi wa jimbo la Songea mjini
kwa ujumla kuitokeza kwa wingi siku ya Januari 13 mwaka huu kumpigia
kura mgombea huyo na kuacha kuendelea kusikiliza na kufuata propaganda
za wagombea wa vyama vya upinzani ambao walio wengi hawajui kilichoko
kwenye vyama hivyo vya upinzani kwa sababu yeye alikuwepo huko na anajua
kulivyo.
Viongozi wengine wa kambi ya upinzani
waliopanda jukwaani katika viwanja vya mikutano vya Majengo na kutangaza
kujiunga na chama cha mapinduzi ni pamoja na aliyekuwa katibu wa chama
cha ACT Wazalendo mkoa wa Kigoma Sharon Msanya ambaye kabla ya kutangaza
kujiunga na chama cha mapinduzi aliwataka wapiga kura wa jimbno la
Songea mjini kutokuthubutu kulifanya jimbo hilo kuwa kambiya upinzani
kwa sababu kufanya ni kurudisha nyuma jitihada za serikali za kuwaletea
wananchi maendeleo ambayo wameyahityaji kwa muda mrefu kurtoka
serikalini na serikali ya awamu ya tano inaendelea kuonesha dhamira ya
dhati kuwafikishia wananchi maendeleo hayo.
Alisema yeye amekuwa kiongozi mkubwa wa
chama cha ACT Wazalendo katika ngazi ya mkoa lwa Kigoma akini amefikia
uamuzi huo wa kusafiri kutoka mkoani Kigoma mpaka mjini Songea ili aweze
kupata fursa ya kuwaeleza wananchi wa Songea umuhimu wa kukiunga mkono
chama cha mapinduzi na mgombea wake Dkt Dams Ndumbaro kwa ajili ya
maendeleo yao na taifa kwa ujumla kwa sababu mgombea huyo amekuwa
mpigania maendeleo ya taifa kwa muda mrefu hata kabla hajafikia uamuzi
huo wa kugombea nafasi hiyo ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo lake.
Huku naye Edna Sunga aliyekuwa katibu
wa kamati ya maendeleo ya jamii taifa na mjumbe wa kamati kuu na
halmashauri kuu taifa wa chama cha ACT Wazalendo akizungumza baada ya
kukihama chama hico na kujijnga na chama cha mapinduzi amesema kwa
sababu yeye ni muumini wa kuzingatia miiko na vita dhidi ya rushwa na
kuwaletea maendeleo wananchi ameona hana sababu ya kuendelea kuwa kwenye
upinzani badala ya kuongeza na kujnganisha nguvu ya kuwajhudumia
wananchi walio wengi.
Amesema kiongozi au mwananchi yeyote
mwenye dhamira ya dhati ya maendeleo ambayo wananchi walio wengi
wanayahitajihana budi kukiunga mkopno chama cha mapinduzi na mgombea
wake ambaye amevaa taswira ya chama hicho na taifa kwa ujumla huku naye
mgombea wa jimbo hilo kwenye uchaguzi huo akiendelea kuwaomba wananchi
wa mji wa Songea kujiktokeza kwa wingi siku hiyo ya uchaguzi kwa ajili
ya kupiga kura kwa chama cha mapinduzi.
Na Nathan Mtega, Jamvi la habari – Songea
No comments