KAMANDA WA POLISI TANGA AZUNGUMZIA BASI SIMBA COACH KUCHOMWA MOTO
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa ufafanuzi kuhusu tukio la kuchomwa moto kwa basi la Simba Coach.
Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza basi hilo limechomwa leo na wananchi wenye hasira kali baada ya dereva wake kumgonga dereva wa bodaboda.
Akizungumza na Michuzi Globu kwa njia ya simu muda huu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe amefafanua ni kweli amesikia taarifa za kuchomwa moto basi hilo lakini halijachomwa mkoani Tanga kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.
Amesema baada ya kuona taarifa za kuchomwa basi la Simba Coach waliamua kufuatilia lakini wamejiridhisha haikutokea kwenye mkoa wao ila basi hilo limechomwa nchini Kenya.
Kamanda Bukombe ameiambia Michuzi Globu kuwa basi hiyo ilikuwa inatoka Mombasa nchini Kenya na taarifa walizonazo limechomwa huko huko nchini Kenya kwani lilikuwa halijaingia kwenye mipaka ya nchi yetu ya Tanzania na hasa mkoani Tanga.
Alipoulizwa iwapo anafahamu namba za basi hilo linalodaiwa kuchomwa moto na dereva aliyekuwa analiendesha ,amejibu wanaendelea kufuatilia kwa polisi wa nchini Kenya na kisha atatoa taarifa kuufahamisha umma.
"Tunaendelea kukusanya taarifa na kwa kuwa limechomwa huko Kenya tunawasiliana na polisi wa huko ili tuwe na uhakika wa taarifa Kamili za tukio hilo.Hatujapata namba za basi.Wananchi wasubiri tutaeleza kwa usahihi tutakapokamilisha kupata ukweli zinazohusu tukio hilo, "amesema Kamanda Bukombe.
TAARIFA KUCHOMWA MOTO SIMBA MTOTO
Mapema asubuhi ya leo katika mitandao ya kijamii zilianza kuzagaa picha zinazoesha basi linaungua moto, na vyanzo vya moto huo ikawa inaelezwa ni wananchi wenye hasira wamechoma moto basi la Simba Coach.
Taarifa hizo zikawa zinadai tukio hilo limetokea Mkoa wa Tanga lakini haikuwa inaonesha ni wananchi wa eneo gani walioamua kuchoma basi hilo.
Pia taarifa hiyo imedai basi limochomwa moto kutokana na dereva wake kugonga dereva wa pikipiki na hivyo wananchi wakaonesha hasira zao kwa kulichoma moto basi hilo.

No comments