Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet
Na Mwandishi
wetu
Mkazi wa
Iringa, Alex Kalinga (26) amejishindia kitita cha sh milioni 161 kwa kubashiri
kwa usahihi mchezo maarufu kwa ‘Perfect 12’ unaondeshwa na kampuni ya mchezo wa
kubahatisha ya M-Bet.
Kalinga
alikabidhiwa kitita chake jana na Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David
Malley kwa kushirikiana na Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.
Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (katikati) akimkabidhi hundi mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga (kulia) ambaye amejishindia kitita cha sh milioni 161. Kuliakushoto ni Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.Malley
alisema kuwa Kalinga alifanikiwa kubashiri sahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17
na kuwa mshindi wao wa droo ya 17 tokea kuanzishwa kwa mchezo wa Perfect 12.
Alisema kuwa serikali imejipatia jumla ya Sh milioni 29
kutoka kiasi hicho cha fedha ambacho ni asilimia 18 kwa mujibu wa sheria.
“Ni faraja
kubwa kuona kijana mwenye umri wa miaka 26 akishinda mamilioni ya fedha kwa kutumia kiasi cha She elfu moja
tu, hii imedhihirisha kuwa M-Bet ni nyumba ya mabingwa, tunawaomba mashabiki wa
soka kuendelea kucheza mchezo wetu ili kujishindia fedha,” alisema Malley.
Mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga 'akipozi' na mfano wa hundi mara baada ya kukabiziwa jana. Kalinga alijishindia kitita cha sh milioni 161.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhiwa fedha zake, Kalinga alisema kuwa hakuamini taarifa ya
kushinda mchezo huo mara baada ya kupokea simu ya kujulishwa kushinda.
“Nina furaha
sana, mimi ni fundi wa kuchomelea mageti ya chuma, sikuwa na kipato kikubwa
pale Iringia Mjini, nitaanza kujenga nyumba na kufungua kiwanda cha kuchomelea
na nyingine kusaidia familia yangu,” alisema Kalinga.
Meneja wa
Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT),
Catherine Lamwai aliwashukuru M-Bet kwa kuendelea vyema na shughuli zake mbali
ya kuwazawadia washindi mara kwa mara.
No comments