VIJANA JIUNGENI NA VIKUNDI VYA MAZOEZI: NAIBU WAZIRI SHONZA
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (mwenye tisheti nyeupe katikati) akiwa katika mazoezi ya jogging na kikundi cha Kawe Jogging Social Club katika sherehe za miaka mitano ya kikundi hicho zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam (aliyenyoosha kidole kushoto) ni Katibu wa Kawe Jogging Social Club Bw.Alhaj Seif Muhere.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana
Shonza (mwenye tisheti nyeupe katikati)akifanya mazoezi ya viungo na
wanachama wa vikundi mbalimbali vya jogging mkoani Dar es Salaam katika sherehe
za miaka mitano ya kikundi cha Kawe Jogging Social Club leo,(kushoto) Katibu wa Kawe Jogging Social Club Bw.Alhaj
Seif Muhere na kulia ni Mwanachama wa Jogging Kawe Social Club Bi Felister
Mwijage.
****************************************
Na Anitha Jonas – WHUSM
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
ametoa wito kwa vijana kujiunga na vikundi vya mazoezi maarufu kama
(Jogging
Club) kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kujikwamua kiuchumi.
Mheshimiwa Naibu Waziri ametoa wito huo katika sherehe za maadhimisho
ya miaka mitano ya Kawe Jogging Social
Club zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo aliwapongeza wanachama wa
Klabu hiyo kwa kuweza kudumu kwa muda wote huo.
“Napenda kuwapongeza
kwa juhudi zenu pamoja na ubunifu mliyoutumia katika kujiongezea kipato kupitia
klabu yenu kwa kuanzisha mgahawa ambao unawaongezea kipato na kukuza uchumi
wenu kwa hakika mmekuwa ni mfano wa kuigwa,”Mhe. Shonza.
Akiendelea kuzungumza
katika sherehe hizo Naibu Waziri huyo amewahakikishia wanaklabu hao ushirikiano
pamoja na kushughulikia maombi yao ya kupatiwa mashine ya maximalipo.
Naye Mwenyekiti wa Kawe
Jogging Social Club Bw. Abdul Risasi alimshukuru Naibu Waziri kwa
kujumuika nao katika sherehe hiyo na kutoa ombi la kusaidiwa kupata mfadhili
atakayeweza kuwasaidia kufanikisha ushiriki wao katika mashindano ya
Kilimarathon yanayotarajia kufanyika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
“Tumekuwa tunashiriki
katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon kwa miaka minne mpaka sasa na Kawe
Jogging Social Club imekuwa ndiyo kikundi pekee nchi nzima ambacho kimepata nafasi ya kuweza kushiriki
mashindano hayo ambapo wanachama wake hukimbia mpaka kilometa 21,”alisema
Bw.Risasi.
Pamoja na hayo Mwenyekiti
huyo aliendelea kutoa wito kwa vijana kujiunga katika vikundi vya jogging kwani
kupitia umoja huo wanaweza kujitengeneza fursa za kiuchumi na kujiongezea
kipato badala ya kukaa vijiweni na kulalamikia hali ngumu ya maisha.
Kwa upande wa mmoja wa
wanachama wa Msasani Jogging Club Bi Asha Said alitoa maoni yake na kusema
jogging clubs ni nzuri kwani zinasaidia kupata marafiki pamoja na kuimarisha
afya.
No comments