Tanzania yatwaa taji la Cana kanda ya tatu kwa mara ya pili mfululizo
Waogeleaji wa timu ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutetea vyema ubingwa wa Cana kanda ya tatu. |
Muogeaji nyota wa Tanzania, Sonia Tumiotto akipigania Taifa lake katika mashindano ya Cana kanda ya tatu. |
Collins Saliboko wa Tanzania akishindana katika mashindano ya Cana Kanda ya Tatu Afrika. |
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akimkabidhi kombe nahodha wa Tanzania, Sonia Tumiotto pamoja a Natalie Sanford mara baada ya kutwaa ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu. |
Makocha wa timu ya Tanzania wakishangilia mara baada ya kutwaa ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu kwa mchezo wa kuogelea. |
Mashindano ya kuogelea yana mashabiki wake, hapo watanzania wakishangilia kwa nguvu kuwapa hamasa waogeleaji katika mashindano ya 'relay'. |
Muogeleaji wa Tanzania, Denis Mhini akichumpa katika mashindano
ya kuogelea ya Kanda ya ya tatu ya Afrika.
|
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana
Shonza (kulia)akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya
(TSA) Leena Kapadia.
|
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha kuogelea (TSA), Thauriya Diria na Katibu Mkuu wake, Ramadhan Namkoveka wakiwa katika pozi la 'ushindi' mara baada ya Tanzania kutetea ubingwa wa Kanda ya tatu wa Cana |
Marin De Villard (katikati) akipozi na waogeleaji wa Kenya
mara baada ya kutangazwa kuwa muogeleaji bora kwa upande wa wanaume.
|
Muogeaji nyota wa Tanzania, Hilal Hilal akipozi na waogeaji
wa Kenya mara baada ya kushinda medali ya dhahabu.
|
Na Mwandishi wetu
Tanzania
imefanikiwa kutetea ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu Afrika baada ya kuibuka
katika nafasi ya kwanza katika upande wa wanawake na wanaume.
Kwa mujibu
wa matokeo yaliyotangazwa juzi, timu ya
Tanzania ilipata jumla ya pointi 1,394 na kufanikiwa kuzishinda timu maarufu na
kali katika mchezo huo, Zambia ambayo ilipata pointi 968 na Kenya iliyomaliza
ya tatu kwa pointi 957.
Uganda ambayo
ndiyo nchi ya kwanza kuandaa mashindano hayo, ilimaliza ya nne kwa kupata
pointi 759 na kufuatiwa na Afrika Kusini iliyopata pointi 469 ma Sudani
iliyopata oint 459 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania,
Swissair, JCDecaux, Coca Cola, Label Promotions, Tanzania Sign Writers, Giraffe
Ocean View, Print Galore na Slipway Hotel.
Katika mashindano hayo ya siku tatu, timu ya wanawake wa
Tanzania ndiyo ilikuwa kali zaidi kutokana na kuundwa na waogeleaji nyokta kama
Sonia Tumiotto ambaye ndiye nahodha na Natalie Sanford.
Mbali ya hao kulikuwa
na nyota wengine kama Maia Tumiotto ambaye anakuja juu kwa kasi, Smriti Gorkan,
Kayla Gouws, Amani Doggart, Tara
Behnsen, Emma Imhoff, Rania Karume , Chichi Zengeni, Anjani Taylor, Anna Guild, Sanne Kleinveld , Angelica Spence, na Tami Triller.
Kwa upande wa wanaume , nyota alikuwa Marin De Villard pamoja
na wakali wengine kama Collins Saliboko,
Joseph Sumari, Denis Mhini, Hilal Hilal,
Adil Bharmal, Judah Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick, Caleb O'Sullivan,
Khaleed Ladha, Matthew Guild , Chris
Fitzpatrick, Harry McIntosh, Dhashrrad Magesvaran na Joseph Sumari.
Kwa upande wa timu ya
Platnum, nayo ilionyesha kuwa kuna nyota wa baadaye wa Tanzania ambapo timu ya
wanawake iliindwa na Shivan Bhatt,
Natalia, Charlotte Sanford, Vanessa
Dickson ), Rebecca Guild, Meredith Boo , Maria Bachmann ), Kayla Temba na Maya Somaiya.
Kwa wanaume walikuwa Aravind Raghavendran, Mohameduwais
Abdullatif (Bluefins), Abraham Kayugwa, Terry Tarimo, Aliasgar Chakera, Zeke Boos , Yuki Omari,
Augustino Lucas , Fallih Ahmed, Carter
Helsby , Ian Lukaza na Emmanuel Stenson.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana
Shonza aliwapongeza waogeleaji wa Tanzania kwa kutwaa ubingwa huo huku akiahidi
kutoa ushirikiano mkubwa kwa chama cha
kuogelea cha Tanzania (TSA).
No comments