Header Ads

ad

Breaking News

Tanzania kuwakilishwa na timu mbili katika mashindano ya Cana kanda ya tatu ya kuogelea



Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Sonia Tumiotto akifanya vitu vyake wakati wa mashindano ya Taifa ya kuogelea.

Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Hilal Hemed Hilal akishindana wakati wa mashindano ya Taifa ya kuogelea.

Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Collins Saliboko akichuana katika mashindano ya Taifa ya kuogelea.

Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Marin De Villard akionyesha uwezo wake wakati wa mashindano ya kuogelea ya Afrika Kusini.

Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Adil Bharmal  akifanya vitu vyake wakati wa mashindano ya kuogelea ya Afrika Kusini.


Na Mwandishi wetu

Tanzania itawakilishwa na timu mbili za kuogelea katika michezo ya kanda ya tatu ya kuogelaa ya Afrika yaliyopangwa kuanza Alhamisi katika bwawa la Hopac la jijini.

Tanzania imepewa nafasi ya kuwa na timu mbili kutokana na kuwa mwenyeji.

Katibu Mkuu wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA, Ramadhan Namkoveka amesema timu ya kwanza imepewa jina la Tanzanite ambayo itakuwa na jumla ya wachezaji 30 na ya pili inajulikana kwa jina la Platinum ambayo itakuwa  na wachezaji 21.

Namkoveka amesema kuwa timu ya Tanzanite itakuwa na wachezaji 15 wanaume na 15 wanawake na ile ya Platinum itakuwa na wachezaji tisa wanawake na 12 wavulana.

Timu hizo zipo kambini Hoteli ya Giraffe chini ya makocha, Alexander Mwaipasi na Michel Livingstone na zinafanya mazoezi yake kwenye bwawa la Hopac kila siku.
 
Wachezaji wanaounda timu ya Tanzanite ni Rania Karume , Chichi Zengeni, Maia Tumiotto, Smriti Gokarn (Sonia Tumiotto, Anjani Taylor ambao wote wanatoka klabu ya DSC, huku wengine ni Natalie Abwooli Sanford (MIS), Anna Guild, Emma Imhoff (MSC), Sanne Kleinveld ( ISM Moshi),  Angelica Spence, Tara Behnsen, Tami Triller,Kayla Gouws na Amani Doggart ambao wanatoka klabu ya Taliss.

Wachezaji wanaume ni Judah Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick, Caleb O'Sullivan, Khaleed Ladha na Matthew Guild wanatoka klabu ya Mwanza, Chris Fitzpatrick (ISM Moshi), Marin DE Villard (DSC), Adil Bharmal, Hilal Hilal, Harry McIntosh, Dhashrrad Magesvaran (Taliss) na wanaotoka klabu ya shule ya kimataifa ya Morogoro ni   Joseph Sumari, Collins Saliboko na Dennis Mhini.

Wachezaji wanaounda klabu ya Platinum kwa upande wa wanawake ni  Shivan Bhatt, Natalia (Taliss), Charlotte Sanford,  Vanessa Dickson (MIS), Rebecca Guild, Meredith Boo (MSC), Maria Bachmann ( ISM Moshi), Kayla Temba na Maya Somaiya  ambao wote wanatoka klabu ya DSC.

Wanaounda timu ya wanaume ni Aravind Raghavendran, Mohameduwais Abdullatif (Bluefins), Abraham Kayugwa( ISM Moshi), Terry Tarimo,  Aliasgar Chakera(Taliss), Zeke Boos (MSC), Yuki Omari, Augustino Lucas (Champion Rise), Fallih Ahmed (Taliss), Carter Helsby (MSC), Ian Lukaza(ISM) na Emmanuel Stenson wa shule ya kimataifa ya Morogoro.

 Namkoveka alisema kuwa mchezaji  Hilal Hilal ambaye yupo kambini Dubai atajiunga na wenzake kesho katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux,  Coca Cola, Label Promotions , Print Galore na Slipway Hotel.
Mbali ya Tanzania, mashindano hayo pia yatashirikisha waogeleaji kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Sudan na Kenya.

No comments