Miss Universe Tanzania kufanyika Jumamosi
Na Mwandishi wetu
Mashindano ya kumsaka mrembo wa
Kiss Universe Tanzania yamepangwa kufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa jijini.
Mashindano hayo yatashirikisha
jumla ya warembo 10 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa mujibu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi.
Maria amewataja mabondia hao kuwa
ni Lilian Maraule , Glory Gideon, Melody Tryphone, Anitha Mlay, Silvia
Mkomwa, Rogathe Ally, Prisca Dastan ambao wote wanatoka Dar es Salaam.
Warembo wengine ni Maureen Foster na Mary Peter wanaotoka Mwanza wakati anayetoka mkoa wa Mbeya Zahra Abdul.
Miss Universe anayemaliza muda wake, Jihan Dimachk
Alisema kuwa warembo hao watakuwa chini ya Miss Universe namba mbili wa mwaka jana, Lilian Loth katika kambi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na SeaCliff Court Residence, Diana Magese, MnM, Kasakana na Bonuzi.
“Maandalizi ya mashindano hayo
yamekamilika na wapenzi wa masuala ya urembo watapata burudani safi
kutoka kwa DDI Dance, poetry group (Romantic), A beautiful song kutoka
kwa Jeff Mduma,” alisema Maria.
Alifafanua kuwa wamedhamilia
kumpata mrembo bora ambaye atarejesha heshima ya mashindano hayo kama
ilivyokuwa kwa Flaviana Matata ambaye alimaliza katika nafasi tano bora
nchini Mexico mwaka 2007.
“Tumefanya uchaguzi wa warembo
vizuri na wengi ni bora, kwa sasa tunawafundisha masuala mbalimbali ya
urembo, lengo ni kuwafanya wawe bora, wote ni washindi, lakini
tunahitaji mshindi mmoja ambaye ataliwakilisha Taifa katika mashindano
ya Kimataifa,” alisema.
Alisema kuwa mashindano hayo pia
yatamtoa mshindi wa taji la Miss Earth Tanzania na mshindi wa taji la
Miss Tourism Queen International wa Tanzania.
No comments