M-Bet yawazawadia washindi nane wa mchezo wa Perfect 12
Msemaji wa Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet, David Malley (kulia) akimkabidhi hundi ya jumla ya Sh milion 153 kwa mmoja wa washindi nane walioshinda mchezo wa Perfect 12, Juma Mhanga (Katikati). Kushoto ni Afisa Kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngollo. Picha
Na Mwandishi wetu
Jumla ya washindi nane wa mchezo wamshinda kitita cha sh milioni 15.6 kila mmoja baada ya kufanikiwa kubashiri timu 12 (Perfect 12) katika bahati nasibu ya kampuni ya M-Bet.
Washidi hao ni Hija Hassan ambaye anatoka Manyara, Batista Rugemalira (Tanga), John Bundla (Shinyanga), Bakari Ally (Manyara), Juma Mhanga (Mbeya), James Tuseko (Sumbawanga), Sabatho Sebastaina (Mara) na Suleiman Suleiman wa Mwanza.
Akizungumza wakati makabidhiano jana, Msemaji wa kampuni ya M-Bet, David Malley alisema kuwa washindi hao wamebatika baada ya kufanikiwa kubahatisha kwa usahihi droo ya ‘Perfect 12 na kujiongezea kipato katika maisha yao.
Malley alisema kuwa droo hiyo inafanyika kila siku na kuwaomba wapenzi wa michezo ya kubashiriki kushiriki ili kujiongezea kipato.
Alifafanua kuwa washindi hao walitakiwa kupata zaidi ya Sh milioni 19 lakini kutokana na kukatwa kodi asilimia 18, walipata kiasi hicho cha fedha ambacho si haba.
“Tunaomba watanzania kucheza mchezo huu ili kuweza kupambana na hali yako kama ilivyo kauli mbiu yetu, michezo yetu ni ya uhakika na tunaamini kila mshiriki atajishindia kipato kikubwa,” alisema Malley.
Mmoja wa washindi, Juma Mhanga alisema kuwa alikesha kusubilia matokeo hayo ambayo yamempa fedha ambayo ataifanyia mambo ya maendeleo katika familia yake.
“Nimefarijika sana, marafiki zangu walinikatisha tamaa ya kutocheza mchezo huu, sikuacha na leo (jana) nimefanikiwa kupata fedha, nilitaongeza mtaji katika biashara zangu,” alisema Mhanga.
They do these interests to benefit their target that driving should not to feel like an extremely troublesome errand but rather substantially more of a pleasing background. bet at home
ReplyDeleteYou can profit different advantages by playing an online clubhouse diversion. voodoodreams
ReplyDelete