BENKI YA TPB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI NA MEZA SHULE YA SEKONDALI UCHILE SUMBAWANGA
Mkurugugenzi
wa Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya TPB, Sosthenes Nyenyembe, akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi viti na meza 50 iliyofanyika Shule ya
Sekondari Uchile iliyopo Sumbawanga vijijini Mkoa wa Rukwa. Msaada huo
umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 3.7.
Mkurugnzi
wa Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya TPB, Sosthenese Nyenyembe (kushoto)
akimkabidhi moja kati ya meza na viti kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Uchile, Wilbroad Lucas (katikati) Sumbawanga Vijijini
Mkoani Rukwa. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Sumbawanga vijijini, Nyingi
Msemakweli. Benki ya TPB ilitoa msaada huo wenye thamani ya milioni 3.7
katika Shule ya Sekondari Uchile, baada ya kupata maombi ya msaada
kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo.
No comments