Tigo yatoa msaada wa mfumo wa kidigitali wa elimu mkoani Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella,akimshukuru Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya(kushoto) baada ya kuzindua programu ya kompyuta yenye vitabu vya masomo ya shule za sekondari(Tigo eSchool) iliyounganishwa kwenye shule ya sekondari Pamba na Kampuni ya Tigo, Jumla ya shule tano za mkoa huo zimeunganishwa na huduma hiyo.
|
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akijaribu huduma ya Tigo eSchool kwenye shule ya Sekondari Pamba mkoani Mwanza. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa, Alli Maswanya (kushoto)na Mbunifu waTovuti toka Shule Direct, Rajabu Mgeni. |
………………………………………………………………
Sekondari tatu za Mwanza zapokea msaada kutoka mradi wa Tigo E-schools
Mwanza 21 Septemba, 2017- Kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania kupitia
mradi wa Tigo E-schools imetoa msaada wa mfumo wa teknologia kwa masomo
kumi na moja (11) ya shule kwa sekondari tatu (3) za Mkoani Mwanza.
Ikiwa ni sehemu ya shughuli za jamii zinazoendana na msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa, msaada
huu unaonesha sifa kuu ya Tigo kama mtandao unaoelewa wateja wake na
kuwapa huduma zinazoendana na mahitaji yao. Kupitia
mradi wa Tigo e-schools, Tigo imeona na kuelewa hitaji la wanafunzi la
maarifa ya Tehama, na inakutana na hitaji hili kupitia utoaji wa
kompyuta zilizounganishwa na intaneti na mifumo mbali mbali ya elimu.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kukabidhi mfumo huo, Meneja Kanda wa Tigo, Ali
Maswanya alisema kuwa mfumo huo utawaandaa wanafunzi kuibua fursa na
kuwa sehemu ya mabadiliko ya Tehama ulimwenguni.
‘Dunia ya sasa inaendeshwa kidigitali. Mradi wa Tigo E-shools unawaandaa wanafunzi kuwa sehemu ya ulimwengu huu wa kidigitali. Kupitia
mfumo huu, wanafunzi wataongeza busara, kupanua mitazamo na ubunifu
wao, na hivyo kuibua fursa pamoja na kukabiliana na changamoto
zinazoendana na ulimwengu wa sasa wa digitali,” Maswanya alisema.
Alitaja
shule za sekondari zilizofaidi kutoka kwa msaada huo Mkoani Mwanza ni
Shule ya Sekondari Pamba, Sekondari ya Mwanza na Sekondari ya Mirongo.
Tigo E-schools pia itasambaza mfumo huo wa elimu kwa shule 52 za
sekondari katika mikoa 12 kati ya mikoa 15 ambayo msimu wa Tigo Fiesta
2017 Tumekusomaa utazuru mwaka huu.
Mwaka
2016, Tigo ilifanya makubaliano na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano kuwezesha kusambazwa kwa mtandao katika shule za sekondari
nchini ili kuchangia mpango wa miaka miwili wa serikali kuleta
mabadiliko ya elimu kwa njia ya mtandao.
Kama
sehemu ya makubaliano hayo, Wizara ilitoa majina ya shule zisizokuwa na
maabara ya kompyuta na pia kutoa mwongozo wa utekelazaji wa mradi huo.
Tigo ilishiriki katika ujenzi na kuunganisha maabara mpya za kompyuta na
mtandao, na hatua ya tatu ni ya kuunganisha shule husika na teknologia
hii ya elimu kwa njia ya mtandao.
“Kupitia
mpango wetu endelevu wa kuwekeza katika hudma za jamii, Tigo inachangia
jitahada za serikali za kuigeuza Tanzania kuwa na uchumi wa maarifa
ifikapo mwaka 2025.” Maswanya aliongeza.
Shule
ambazo zitaunganishwa na mfumo huo wa elimu kwa njia ya Tehama ni
Arusha Day, Ilbouru na Arusha Sekondari mkoani Arusha; Mwanza, Pamba na
Mirongo Sekondari mkoani Mwanza; Tabora Girls na Milambo Sekondari
mkoani Tabora; na Mpwapwa Sekondari mkoani Dodoma.
Shule
nyingine ni Iringa na Kleruu Sekondari mkoani Iringa; Matalawe na
Songea Girls Sekondari mkoani Songea; Njombe na Mpechi Sekondari mkoani
Njombe; Morogoro Municipal na Mzumbe Sekondari zilizopo Morogoro; pamoja
na Handeni na Shemsanga Sekondari huko Tanga.
Shule
nyingine zitakazofaidi mfumo huu wa elimu kutoka Tigo e-schools ni
Lyamungo Sekondari na Machame Girls Sekondari huko Moshi; Newala Day na
Masasi Day Sekondari zilizopo Mtwara na kwa mkoa wa Dar es Salaam, sekondari za Mbagala, Kibamba, Benjamin Mkapa na Makumbusho zitaunganishwa na mfumo huo wa elimu kwa njia ya Tehama.
‘Kwa
mara nyingine, natoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa
kuiruhusu Tigo Tanzania kuwa sehemu ya mipango yake ya kuiingiza
Tanzania katika mfumo wa uchumi wa maarifa,’ Meneja huyo wa Tigo
alimaliza.
Tigo
ni mdau muhimu wa elimu na imetoa michango mbali mbali kuinua viwango
vya elimu nchini. Mwaka jana Tigo ilichangia madawati zaidi ya 7,100
katika shule za mzingi nchini kote. Vilevile Tigo imetoa kompyuta 77
zilizounganishwa na mtandao wa kasi zaidi wa Tigo kwa vituo vya elimu ya
juu nchini.
No comments