NDANTO FC MABINGWA TULIA CUP 2017

Beki wa timu ya Isange Fc, Zawadi
Andombwisye (kushoto) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Ndanto
Fc, Erick Mwangoye, wakati wa mchezo wa Fainali za ‘Tulia Cup’
uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani
Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1
na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5

Beki wa timu ya Ndanto FC, Fidelis
Yeo (kulia), akiwania mpira na mshambuliaji wa Isange FC, Hussein Thom,wakati wa mchezo wa fainali za ‘Tulia Cup’ uliochezwa jana Septemba 21, 2017
kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Katika
mchezo huo Ndanto ilishinda mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa
mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5

Wachezaji wa Isange Fc, Shadrack
Kandrum (kushoto) na Hussein Thom (kulia) wakimdhibiti Mandela Chaile,
wakati wa mchezo wa fainali za ‘Tulia Cup’ uliochezwa jana

Beki wa timu ya Isange Fc, (kulia)
akimdhibiti mshambuliaji wa Ndanto Fc, Julius Mtawala, wakati wa mchezo
wa Fainali za ‘Tulia Cup’ uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja
wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto
walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na
kitita cha sh. milioni 1.5.



Nahodha wa timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyoundwa na wachezaji kutoka kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji Amina Juma Kizaba akipokea kombe la ushindi wa kwanza kutoka kwa Mdadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali James A. Mwakibolwa jana Tukuyu Mbeya baada ya kuilaza timu pinzani ya Kiimo Kijiji Kitulivu (KKR) kwa mabao 26-16.

Mkuu wa Majeshi mstaafu, Davis
Mwamunyange,
akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Netiboli ya Wizara ya Mambo ya
Ndani, baada ya kushika nafasi ya kwanza katika fainali za ‘Tulia
Cup’kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Majeshi mstaafu, Davis
Mwamunyange, akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Isange, Frank Asilih,
baada ya kushika nafasi ya pili katika fainali za ‘Tulia Cup’kwenye
uwanja wa Tandale Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya
(Picha na Muhidin Sufiani)
No comments