Zimbabwe mabingwa Cosafa 2017
Rustenburg, Afrika Kusini
TIMU ya taifa ya Zimbabwe imetwaa Kombe la Cosafa kwa mara ya tano, baada ya kuilaza Zambia mabao 3-1 katika mechi ya fainali iliyopigwa Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace, Rustenburg jana usiku.
Zimbabwe imekuwa timu bora katika michuano hiyo, ikicheza mechi sita katika siku 14 na kufunga mabao 19.
Ilikuwa kazi ngumu kwa Zambia, ambayo ilitinga hatua ya robo fainali kwa jasho, lakini hakuweza klujiamini kama kwa Zimbabwe.
Knox Mutizwa aliifungia bao la kwanza Zimbabwe dakika ya 22, lakini likiwa la tano katika michuano hiyo, lakini Paul Katema aliisazishia Zambia bao hilo dakika ya 39.
Zimbabwe ilifanikiwa
kupata bao la pili lililofungwa na Talent Chawapiwa dakika ya 56, kabla ya
Ocean Mashure kuifungia timu yake ya taifa bao la tatu dakika ya 67.
Nahodha wa Zimbabwe, Ovidy Karuru ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo mwaka huu, akikwamisha wavuni mpira mara sita, akizmidi Knox Mutizwa.
No comments