Header Ads

ad

Breaking News

Watu 8 wapatikana wamekufa ndani ya lori Marekani

 Polisi wa San Antonio wakidhibitisha idadi ya mili iliyopatikana. (San Antonio Police Department)
 
Watu wanane wamepatikana wamekufa ndani ya lori lililokuwa limeegeshwa nje ya duka la Walmart huko San Antonio katika jimbo la Texas nchini Marekani kwa mujibu wa polisi.


Watu wengine 20 walikuwa katika hali mahututi wengine wakionekana kukumbwa na mshutuko wa joto na kuishiwa na maji mwilini walipelekwa hospitalini.

Polisi hawakusema penye lori hilo lilitoka lakini walisema kuwa dereva amekamatwa.
Wanachunguza ikiwa ni kisa cha kuwasafirisha watu kiharamu.

Idara ya uhamiaji nchini Marekani inajaribu kubaini watu hao ni kutoka wapi.
Jimbo wa San Antonio liko umbali wa kilomita chake kutoka mpaka wa Mexico.

Polisi walisema kuwa miili hiyo iligunduliwa kufuatia simu iliyopigwa na mfanyakazi wa Walmart ambaye alikuwa ameombwa maji na kutoka kwa lori hilo.

Kanda ya video kutoka duka la Walmart ilionyesha magari kadha yaliyowasili kuwabeba manusura.

No comments