Upinzani Zimbabwe wamtaka Mugabe ajiuzulu
Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao
Vyama vya upinzani
nchini Zimbabwe vimerejelea wito wao wa kutaka Rais Robert Mugabe mwenye
umri wa miaka 93 ajiuzulu, na kumlaumu kwa kuiongoza nchi kutoka
hospitalini kufuatia madai kuwa alisafiri kuenda Singapore kwa matibabu.
"yeye bado si kijana mdogo, njia hii anajiadhibu sio nzuri kwa afya yake ya kimwili na kiakili.
Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe kusonga mbele chini ya uongozi mpya."
Karauone Chihwayi, msemaji wa upande uliojitoa MDC naye alitoa matamshi kama hayo.
"Nchi hii imekwama leo hii kwa sababu rais wa Zanu anaongoza akiwa kitanda cha hospitali."
Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao licha ya kuonekana kutokuwa na afya nzuri na amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.
No comments