Ufyatuaji risasi watokea kwenye ubalozi wa Israel nchini Jordan
Vikosi vya usalama vimefunga barabara eneo hilo. (AFP)
Watu wawili raia wa
Jordan wameuawa na muisrael mmoja kujeruhiwa wakati wa kisa cha
ufyatuaji risasi kwenye ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Jordan
Amman.
Ripoti chache zimetolewa kuhusu kile kilisababisha kutokea kwa ufyatuaji huo wa risasi.
Vikosi vya usalama vimezingira ubalozi huo na utawala wa Israel umewahamisha wafanyakazi.
Ufyatuaji huo ulitokea katika jengo moja linalotumiwa na ubalozi wa Israel.
Mamlaka za Israel hazijazungumzia kisa hicho.
Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman.
Siku ya Ijumaa maelfu ya watu waliandamaa mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem. BBC
No comments