Sundowns, USM zatinga robo fainali Afrika, Zamalek yatupwa nje ya michuano hiyo
USM Alger ya Algeria na Al Ahly
Tripoli ya Libya zimetinga hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika, huku
mshindi wa pili wa michuano hiyo mwaka jana, Zamalek ya Misri ikitupwa nje ya
michuano hiyo.
Ushindi wa mabao 4-1 nyumbani dhidi
ya Caps United ya Zimbabwe jijini Algiers na kuihakikisha USM kukaa kileleni
mwa Kundi B kwa kujikusanyia pointi 11 katika michezo sita iliyocheza.
Ahly Tripoli ilifanikiwa kuwabana
mabingwa mara tano wa kombe hilo, Zamalek kwa kutoshana nguvu kwa mabao 2-2 jijini Cairo
na kufanikiwa kufikisha pointi tisa.
Tayari, Esperance ya Tunisia imekamata
nafasi ya kwanza Kundi C, baada ya kuilaza Saint George ya Ethiopia mabao 4-0 mjini
Tunis.
Mamelodi Sundowns ya South Africa, ambayo
pia ilikata tiketi ya kucheza robo fainali, ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya V
Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) mjini Pretoria.
Etoile Sahel ya Tunisia, Ferroviario
Beira ya Msumbiji, Wydad Casablanca ya Morocco na bingwa mara nane wa michuano
hiyo, Al Ahly ya M isri zimekata tiketi ya kucheza robo fainali.
No comments