Rooney atua rasmi Everton
Mshambuliaji wa
Manchester United na mshikilizi wa rekodi ya mabao Wayne Rooney
amejiunga na Everton, miaka 13 tangu aihame klabu hiyo.
Alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mara tano tangu aihame Everton kwa pauni milioni 27 mwaka 2004.
"Ninahisi vizuri kurudi, sitangoja kukutana na wenzangu, kuingia mazoezini na kisha kuingia uwanjani kucheza," alisema Rooney.
Rooney anarejea Everton wakati Man United ikikamilisha usajili wa mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku kwa pauni milioni 75.
No comments