PLUIJM AFUNGA USAJILI SINGIDA UNITED NA MKONGWE KIGI MAKASI
Kocha Mholanzi Hans van der Pluijm (kulia) akimkabidhi jezi ya Singida United, Kigi Makasi (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili. |
Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO
anayeweza kucheza kama beki pia, Kigi Makasi, amekamilisha uhamisho
wake kutoka Ndanda FC kujiunga na timu mpya katika Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, Singida United FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Kocha
Mkuu wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm amemkabidhi jezi
Kigi leo aanze maisha mapya ya soka baada ya kuchezea Yanga, Simba na
Ndanda FC.
Mtendaji
Mkuu wa Singida United, Sanga Festo leo ameiambia Bin Zubeiry Sports –
Online kwamba Kiggi anafanya idadi ya wachezaji wa Singida United kufika
25, kati yao 16 wakiwa ni wapya waliosajiliwa kutoka timu mbalimbali,
wakati tisa walikuwemo kwenye vita ya kupandisha timu Ligi Kuu kutoka
Daraja la Kwanza.
Sanga
amesema wamepata mchezaji mzuri anayeongoza kwa moyo wa kujituma
vilivyo uwanjani, Makasi ambaye ameamua kujivua beji ya Unahodha wa
Ndanda FC na kuhamia katikati ya nchi ya Tanzania kuungana na timu ya
Ushindi, SU.
Ikumbukwe
Singida United ilianza kwa kukamilisha usajili wa wachezaji saba wa
kigeni kwa mujibu wa kanuni, ambao ni Elisha Muroiwa, Twafadzwa Kutinyu,
Simbarashe Nhivi na Wisdom Mtasa wote kutoka Zimbabwe, Shafik Batambuze
kutoka Uganda, Dany Usengimana na Michel Rusheshangoga kutoka Rwanda.
Wachezaji
wengine wapya wazawa mbali ya Kigi ni Atupele Green kutoka JKT Ruvu,
Miraj Adam kutoka Africa Lyion, Kenny Ally kutoka Mbeya City, Roland
Msonjo kutoka Mshikamano FC, Pastory Athanas kutoka Simba, Ally Mustafa
‘Barthez’, Deus Kaseke kutoka Yanga na Salum Chuku kutoka Toto Africa.
“Tunawashukuru
vilabu mbalimbali ambao tulifikia makubaliano nao na wamewachukua
baadhi ya wachezaji wetu walioipandisha timu, na baadhi ya wachezaji
waliomba kuondoka kwa ridhaa yao,”amesema Sanga.
www.binzubeiry.co.tz
No comments