Mwakilishi wa Jimbo la Tungu Simai Mohammed, Mbunge wa jimbo hilo, Khalifa Salum washiriki ujenzi wa Soko la Samaki katika Kijiji cha Tindini
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe
Khalafa Salum Suleima wakishiriki katika ujenzi wa Taifa wa kujenga Soko
la Samaki katika ufukwe wa pwani ya Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu
Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja, wakikata majengo ya kuezekea bati katika
soko hilo. Pia wamekabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi huo ili kutowa
mazingira mazuri ya Soko hilo wakati wa kufanya mnada wa samaki kwa
wavuvi wanaporudi baharini kuvua.
Wananchi wa Kijiji cha Tindini
Unguja Ukuu wakishirikiana na Mbunge wao na Mwakilishi katika ujenzi wa
Taifa wa Soko la Samaki katika ufukwe wa Bahari ya Unguja Ukuu Zanzibar.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmtJPsx3useMpgZe5R6ZBcwg43dItG0NMawh4QSkTMvQauadzEHReZc1IZy08Fq8B_kvaIjDmYW3iSEIYkam5rY5LuwvAn6luDdEJn9sAx8BmDHv6qM7mO5nR37vUEr6s3MQNNv0WO5aA/s640/DSC_0707.JPG)
Mbunge nas Mwakilishi wa Jimbo
la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said ma Mhe Khalifa Salum
Suleiman wakikabidhi mabati kwa Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja
Bi. Sauda Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ya Mabati hayo na miti
yamefanyika katika viwanja vya Soko hilo Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu
Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini.
Wananchi wa Kijiji cha Tindini
wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua
ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki
wao..
Wananchi
wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki
Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa
kijiji hicho kuuzia samaki wao
Kiongozi wa Kijiji cha Tindini
akitowa maelezo ya ujenzi wa Soko hilo la Samaki katika ufukwe wa bahari
yao litakalotowa huduma ya kuuzia samaki kwa wavuvi katika soko la
mnada.
Mwakilishi wa Jimbo las Tunguu
Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Soko la
Samaki katika kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja na
kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitumia soko hilo kwa shughuli zao za
biashara ya samaki na minada kwa wavuvi wanaorudi bahari kuvua.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo kwa Wananchi wa Jimbo lake.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi
Mkoa wa Kusini Unguja Bi Sauda Ramadhani akizungumza wakati wa hafla
hiyo ujenzi wa taifa na kukabidhi mabati na vifaa vya ujenzi wa Soko la
Samaki katika Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.
Wananchi na wavuvi wa kijiji
cha Tindini Unguja Ukuu wakimsikiliza mgeni rasmin wakati wa hafla hiyo
ya ujenzi wa Taifa na kukabidhi mabati kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa
Soko hilo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini
Unguja akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge na Mwakilishi na Wananchi
wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu baada yas hafla hiyo.
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspots.com
Zanzinewes.com.
Email.othmanmaulid@gmail.com
No comments