MKE WA WAZIRI MKUU AWASIHI WANAFUNZI KUTOKATISHA MASOMO
MKE
wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewasihi wanafunzi wa kike nchini
kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo yao.
Amesema
ni vema wanafunzi hao wakatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa
mfululizo kutoka kiwango kimoja cha taaluma kwenda kingine.
Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 23, 2017) alipozungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Vwawa wilayani Mbozi.
Mke wa
Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika
ziara ya mkoa Songwe, aliwaasa wanafunzi hao kutumia wakati huu kwa
kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo viovu.
“Nawasihi
mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara kwa ajili ya
kujenga maisha yenu ya baadae. Msikatishe masomo yenu.”
Mama Mary aliongeza kwamba “utumieni muda huu vizuri ili msije mkaujutia baadae, kwani wakati ni mali ukipita umepita.”
Alisema
ni vizuri wakasoma hadi chuo kikuu na kwamba wasikimbilie kufanya mambo
yasiyowahusu kwa sasa kwani mshika mawili moja lazima limponyoke.Mke
wa Waziri Mkuu alisema wanafunzi hao wakisoma hadi elimu ya juu
watakuwa na uwezo wa kutambua jambo lipi ni jema na lipi ni baya.
“Kilichonifurahisha
zaidi ni kwa sababu mimi pia ni mwalimu kwa hiyo inavyoona wanafunzi
wako vizuri kama hivi nafurahi sana, hivyo nawaomba msome kwa bidii.”
Serikali imetunga sheria kali dhidi ya watu wanaosababisha watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kuwapa mimba au kuwaoa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JULAI 24, 2017
No comments