Manchester United yaichapa Real Madrid kwa penalti
Andreas
Pereira wa Manchestern United (kushoto) na winga wa Real Madrid Gareth Bale,
wakati wa mechi ya Kombe la kimataifa iliyopigwa usiku wa kuamkia leo nchini
Marekani. (AFP/Getty Image)
MIAMBA ya Ligi Kuu England, Manchester United wameifunga Real Madrid kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.
Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari.
Penalti saba kati ya kumi hazikuingia nyavuni.
United wameshinda michezo yote minne katika ziara nchini Marekani na watakutana na Barcelona katika fainali siku ya Jumatano.
No comments