WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA NYUMBA YAO KUANGUKIWA NA MTI
Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo |
Vero Ignatus,Arusha
Kutokana na mvua inayonyesha mfululizo Mkoani Arusha imeleta maafa makubwa katika familia ya mzee Jonathani Kalambiya (55), mkazi wa sokoni II katika kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru mkoani Arusha baada ya mti
mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.
mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.
Mkasa
huo wa usikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku baada ya mti huo
kung’olewa na maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa jira na mti huo.
Kamanda
wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto
wawili wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dr
Mohamed ya jijini Arusha.
Mkumbo
aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya
tukio alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa
kidatu cha pili wa shule ya sekondari ya Inaboishu.
Kamanda
alimtaja mwanafunzi mwingine ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia
Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani
Arumeru mkoani Arusha.
Amesema
watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo
aliyetambuliwa kwa jina la Giliad Jonathani(31), Lazaro Lomnyaki
(26) na Best Jonathani(20).
(26) na Best Jonathani(20).
Kamanda
Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana
uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea
kunyesha katika Jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla.
Alisema
na kuitakia pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi
makubwa sana kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na
uvumilivu katika wakati huu mgumu kwake.
Kamanda
Mkumbo ametoa wito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari
katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati
nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.
Amesema
kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga
mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali
hiyo.
Aidha
kamanda ametoa tahadhari kutokana na habari za uzushizinazoendele kuwa
jana kwenye kuaga miili ya wanafunzi kuna mtu alidondoka juu ya mti na
kufariki pamoja na mama mmoja mtoto wake mdogo alifariki,amesema habari
hizo siyo za kweli wananchi wazipuuze kabisa
nyumba ikiwa imeangukiwa na mti kama inavyoonekana
katika picha
katika picha
Mti ulioanguka ukang’ookana shina lake na kuangukia nyumba na kusababisha
maafa hayo ya watu watano wa familia moja.
maafa hayo ya watu watano wa familia moja.
Jitihada za uokozi zikiendelea
Miili ikiwa imeshapakiwa ndani ya gari la polisi
No comments