WAKUU WA WILAYA, WAKURUGENZI ZINGATIENI MIPAKA YA MADARAKA YENU-MAJALIWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Serikali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya
na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa baada ya kufungua
mafunzo hayo katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Kulia
kwake ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Selemani Jafo na kushoto
kwake ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja.
Aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina
Mndeme.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme baada
ya kufungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
za Seriklali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017.
Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI,
Selemani Jafo na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa
Joseph Semboja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja
baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa
Halmashauri za Serikali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma
Mei 9, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,
Selemani Jafo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini
kuzingatia mipaka ya madaraka yao na kuhakikisha hatua wanazochukua
katika utendaji wao zinafuata Sheria ,Kanuni na Taratibu katika
Utumishi wa Umma.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne,
Mei 9, 2017) wakati akifungua mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi
wa Halmashauri za Wilaya katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Amesema viongozi hao wanatakiwa
kusimamia kikamilifu nidhamu katika Utumishi wa Umma kwa sababu wenyewe
ni kioo katika kuishi kwa kuzingatia miiko ya Utumishi wa Umma.
Aidha,Mh. Waziri Mkuu amesema
mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo na kuendelea kuwaimarisha zaidi
katika kusimamia shughuli za Serikali na maendeleo kwenye maeneo yao.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amewataka viongozi hao kutoa kipaumbelea katika kufuatilia na
kusimamia kwa makini sekta za afya, kilimo, elimu na maji kwa kuwa ndizo
zinazogusa zaidi maisha ya wananchi .
Pia amewaelekeza wasimamie na
kuziba mianya yote ya upotevu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za
afya na kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na kusimamia
usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo yao.
Kwa upande wake Naibu Waziri
Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI,
Mheshimiwa Suleiman Jafo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha
viongozi hao wanapata mafanikio makubwa katika utendaji wao wa kazi ili
Serikali iweze kupata tija.
Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja alisema wametoa mafunzo kwa
viongozi hao ili kuwajengea uwezo wa kuongoza kwa kuwa mazingira ya
kufanyia kazi na mbinu za kungoza zinabadilika.
Alisema mafunzo hayo yatatolewa
kwa awamu nne kupitia kanda nne tofauti ambapo awamu ya kwanza imeanza
na kanda ya kati na imehusisha mikoa sita ya Dodoma, Kigoma, Katavi,
Tabora, Morogoro na Singida na awamu nyingine zitakamilika mwishoni mwa
mwezi Agosti mwaka huu.
No comments