TMEA Yazijengea Uwezo, Bidhaa Kuingia Masoko Kimataifa.
Mwandishi Wetu
Taasisi ya TradeMark
East Africa, inazijengea uwezo bidhaa za Tanzania, kuingia kwenye masoko ya
kimataifa, kwa kuziwezesha kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa, ili ziweze
kuhimili ushindani wa kimataifa na kuingia kwenye masoko ya Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Bara la Afrika na masoko ya kimataifa yakiwemo masoko ya
Ulaya na Marekani.
Mkurugenzi wa TradeMark
Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, zoezi la kuhakikisha bidhaa za
Tanzania zinafikia viwango vya ubora wa kimataifa, linafanywa kwa kupitia
kuendesha mafunzo ya viwango vya ubora kwa kuzitumia taasisi za TBC, TFDA na GS 1 kwa ajili ya barcode kwa bidhaa za
Tanzania, hivyo bidhaa hizo kuweza kuhimili ushindani katika masoko ya
kimataifa kwa kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa.
Ulanga amesema, mafunzo hayo yanaendeshwa kwa awamu
mbalimbali, ni sehemu ya utakelezaji wa mradi mkubwa wa Taasisi ya Trademark
East Africa ujulikanao kama “Women in Trade” unaolenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara
wanawake wa Tanzania, kuhimili ushindani
wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha
wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha
bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa
ambapo Taasisi ya TradeMark imetenga Dola za Marekani zaidi ya Milioni
5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania kugharimia
mpango huo.
Ulanga amesema walengwa
wa mafunzo ya awamu hii ni wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, walio chini ya
mwamvuli wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania , (Tanzania Women
Chamber of Commerce, TWCC), ambapo mafunzo ya mwanzo ilikuwa ni kuwajengea
uwezo ili kuweza kuvuka mipaka na kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia
masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hata nje ya bara la Afrika,
lakini mafunzo ya sasa ni kuwajengea uwezo wa kukidhi viwango vya ubora wa
kimataifa.
Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi
inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti
umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na
wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia,
vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo
TradeMark imeamua kuanza kwa kumkomboa
mwanamke kupitia Chama cha
Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, TWCC, kimepatiwa shilingi milioni 500 kwa
ajili ya kuendesha shughuli zake, ikiwemo kuendesha mafunzo hayo nchi nzima.
“Ukimuwezesha mwanamke, ni kuiwezesha familia nzima, familia
zikiwezeshwa ni kuwezesha jamii nzima na jamii zikiwezeshwa na kuwezesha taifa
kwa ujumla, hivyo uwezeshaji huo kwa
wanawake ni uwezeshaji kwa taifa kupata maendeleo” Alisema Bw. Ulanga.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa TWCC, Bibi, Jaquline Mneney Maleko,
amewasisitiza wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuzichangamkia fursa za
kuwajengea uwezo, zinazotolewa na TWCC kwa udhamini wa Trademark East Africa,
Bi Maleko amewaasa wanawake kutafuta zaidi elimu ya ujasiliamali na sio tuu
kujikita kwenye kutafuta pesa, mwanamke aliyeelimika, anakuwa na uwezo wa
kufanya biashara kubwa zaidi hivyo kutengeneza fedha zaidi kuliko mwanamke
asyeelimika
Mkurugenzi wa TWCC,
Wakili Nourine Mawalla, amesema wanawake wa Tanzania wanajituma sana katika
ujasiliamali wa uzalishaji wa bidhaa bora, lakini bidhaa zao zimekuwa zikikosa
masoko ya kimataifa kutokana na kukosa viwango vya ubora wa kimataifa, hivyo kupitia TWCC na TMEA,
wanawajengea wafanyabiashara, wanawake wa Tanzania, uwezo wa kikidhi viwango
vya ubora wa kimataifa, hivyo bidhaa za Tanzania kukubalika katika masoko ya
Kimataifa,
Bi Mwala ameishukuru TradeMark kwa ufadhili wa mafunzo hayo na
kueleza uwepo wa soko la Afrika Mashariki ni fursa, hivyo Chama cha TWCC,
kinaishukuru TMEA kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania,
kuchangamkia fursa za soko hilo, kufuatia wanawake ndio idadi kubwa ya
wafanyabiashara, lakini wengi huishia kufanya biashara ndogo ndogo kutokana na
kuwa na uwezo mdogo, hivyo chama hicho kinawajengea uwezo na kuwafungulia fursa
za kupata mitaji mikubwa, na kuingiza bidhaa zao kwenye soko la Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa.
TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo
kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi
za kiraia.
TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa masoko, kuboresha mazingira ya biashara, na kuboresha biashara ya ushindani hivyo kuongezeka kwa kiwango cha biashara hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini nakuleta maendeleo ya taifa la Tanzania.
TMEA ina makao
yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina
matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na
Kigali.
Mkurugenzi wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, John Ulanga |
Washirika wa mafunzo hayo.
|
Washirika wa mafunzo hayo.
|
Washirika wa mafunzo hayo
|
No comments