TANZANIA YASHIKA NAFASI YA TATU AFRIKA KWA SHERIA BORA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA KEMIKALI
Mkemia
Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele akiwaeleza waandishi wa habari
kuhusu Tanzania kushika nafasi ya tatu barani Afrika kwa kuwa na Sheria
bora ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali hali iliyopelekea Taasisi hiyo
kuwa moja ya Taasisi bora zenye maabara ya kisasa.Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Huduma ya Ubora wa Bidhaa, Daniel Ndiyo na kushoto
ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, George Kasinga.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Huduma ya Ubora wa Bidhaa, Daniel Ndiyo akiwaeleza
waandishi wa habari umuhimu wa wananchi kupata taarifa na maamuzi ya
mkutano wa Kimataifa kuhusu Udhibiti wa kemikali na kemikali taka
uliofanyika hivi karibuni Geneva, Uswisi kuanzia Aprili 24 hadi Mei 5 mwaka huu.
Meneja
wa Kanda ya Kaskazini GCLA, Christopher Anyango akifafanua kuhusu
mkakati wa Serikali kuwajengea uwezo wananchi kuelewa madhara yatokanayo
na kemikali ambazo zimepigwa marufuku. (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Tanzania
imeshika nafasi ya tatu barani Afrika ikiongozwa na nchi ya Afrika
Kusini na Nigeria kwa kuwa na Sheria bora ya Usimamizi na Udhibiti wa
Kemikali.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali
(GCLA), Prof. Samweli Manyele alipokua akizungumza na waandishi wa
habari juu ya mkutano wa Kimataifa wa Udhibiti wa Kemikali na Kemikali
Taka uliofanyika Geneva, Uswisi kuanzia Aprili 24 hadi Mei 5 mwaka huu.
Prof.
Manyele amesema kuwa katika Bara la Afrika Tanzania ndio nchi pekee
ambayo ina taasisi ya Serikali inayosimamia kemikali wakati nchi zingine
usimamizi wa masuala ya kemikali upo katika taasisi za mazingira kitu
ambacho kinapelekea usimamizi hafifu wa kemikali hizo.
“Tanzania
ni nchi pekee Afrika ambayo taasisi inayohusika na masuala ya kemikali
ipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
na pia ni taasisi yenye kusimamiwa na wataalamu wa kemikali waliobobea
pamoja na kuwa na maabara kubwa inayojulikana kimataifa,”alisema Prof.
Manyele.
Akiongelea
kuhusu mkutano huo, Prof. Manyele amesema kushiriki katika mkutano huo
ni jambo la kisheria hivyo kupeleka watumishi watatu kutoka kwenye
taasisi hiyo inadhihirisha kuwa Tanzania imetimiza majukumu yake kama
Taifa.
Amefafanua
kuwa mkutano huo unaisaidia taasisi kutoa taarifa kuhusu utendaji kazi,
kujifunza nchi zingine wanafanyaje kazi zao, kupata majibu ya moja kwa
moja pamoja na kujadiliana namna ambavyo wataboresha utendaji kazi.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma ya Ubora wa Bidhaa, Daniel
Ndiyo ametaja wadau wanaotakiwa kupata taarifa na maamuzi ya mkutano
huo kuwa ni wafanyabiashara, watumiaji wa kemikali hizo pamoja na
mamlaka mbali mbali za usimamizi wa kemikali.
Naye
Meneja wa Kanda ya Kaskazini GCLA , Christopher Anyango amesema mkutano
huo unawasaidia wananchi kupata msaada wa haraka kutoka katika Ofisi ya
Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuwa wana uelewa pamoja na kupata mafunzo
ya kemikali zinazoruhusiwa na zisizoruhusiwa kulingana na mahitaji kwa
wakati husika.
Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilishiriki katika mkutano huo wa utekelezaji
wa mikataba mitatu ikiwemo ya usafirishaji wa taka sumu kimataifa
(Basel), mkataba unaohusu kemikali zenye madhara na zinazochukua muda
mrefu kuoza katika mazingira (Stockholm) pamoja na mkataba wa Rotterdam
unaohusu upashanaji taarifa juu ya kemikali hatari na viuatilifu katika
biashara ya kimataifa.
No comments