Header Ads

ad

Breaking News

SERIKALI YATENGA BILIONI 30 KAMA FIDIA KWA WAKAZI WA KIPUNGUNI

Naibu Waziri, Edwin Ngonyani 
Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi,na Mawasiliano imetenga Shilingi bilioni thelathini(30) katika mwaka wa fedha 2017/2018 ili kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi wa Kipunguni wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege.
 
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea Mhe.Bonnah Kaluwa.

“Ni kweli Serikali ilifanya uthamini wa mali za wananchi ili kupisha upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam mwishoni wa miaka ya 90 ambapo maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya upanuzi huo ni Kipawa,Kigilagila na Kipunguni”,Alisema Mhe.Ngonyani

Ameongeza kuwa kutokana na gharama za fidia na uhaba wa fedha,Serikali imekuwa ikilipa fidia kwa wakazi hao kwa awamu.Ambapo Mwaka 2009/10 wakazi wapatao 1500 wa eneo la Kipawa walilipwa fidia zinazofikia shilingi bilioni 18 ambapo zoezi hilo lilikamilika Januari 2010.

Katika mwaka wa Fedha 2010/2011 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 12 za fidia kwa wakazi 864 wa Kigilagila na Malipo yalikamilika Januari 2011.Katika mwaka 2013/14 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 1.2 ikiwa ni fidia kwa wakazi 59 kati ya wakazi 801 kwa eneo la Kipunguni.

Aidha katika malipo hayo ni wakazi 742 wa Kipunguni ndio ambao hawajalipwa fidia zao zenye thamani ya takribani 19.“Mwaka wa Fedha 2016/17 Serikali imetenga Shilingi Bilioni tano kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi hao wa Kipunguni”Alisisitiza Mhe.Ngonyani.

No comments