MTIHANI HIMID MAO KESHO ATACHEZA MECHI YA KIRAFIKI YA KWANZA
Kiungo
mkabaji wa Azam FC, Himid Mao, kesho Jumanne anatarajiwa kucheza mchezo
wake wa kwanza wa majaribio akiwa na kikosi cha akiba cha timu ya
Randers, inayoshiriki ligi kuu ya nchini Denmark.
Himid
ambaye aliondoka nchini wiki iliyopita kwenda nchini humo ambapo muda
mrefu alikuwa akitakiwa na timu ya Mamelods Sundowns ya Afrika kusini,
amechagua kwenda Denmark kutokana na kuamini kwamba ndiyo sehemu sahihi
kutimiza ndoto zake ambapo atafanya majaribio hayo kwa muda wa siku
kumi.
Skauti
mkuu wa kusaka vipaji wa timu hiyo, Rasmus Bertelsen, alisema kuwa
kiungo huyo atakuwepo katika mechi hiyo ya kikosi cha akiba cha timu
hiyo kabla ya kuamua kumsajili.
“Himid
lazima awe sehemu ya klabu yetu katika mechi ya wachezaji wa akiba
dhidi ya AC Horsens ambayo itachezwa kesho Jumanne, naamini ataonyesha
kile ambacho tunakitegemea kutokana na uwezo wake.
“Nadhani
tunatarajia kumsajili katika timu yetu kwa sababu kabla ya kuja hapa,
tulikuwa tunamfuatilia, ndiyo maana kwanza majaribio yake yalianzia
katika timu ya vijana kabla ya kumpandisha ili acheze mchezo wa kesho,”
alisema Bertelsen.
No comments