Header Ads

ad

Breaking News

Mourinho: Manchester United hatubahatishi Europa League

Kocha wa Manchester, Jose Mourinho
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwamba haamini kwamba anacheza kamari kwa kuangazia zaidi ubingwa wa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

Meneja huyo, ambaye ameamua kuangazia ligi hiyo badala ya kumaliza katika nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia, anasema uamuzi wake ni wa busara.
United wanaongoza 1-0 dhidi ya Celta Vigo nusufainali kutoka kwa mechi ya kwanza wanapoelekea kwa mechi ya marudiano leo Alhamisi jioni uwanjani Old Trafford.
Mourinho amesema kuwepo kwa mechi nyingi ambazo klabu yake inahitajika kucheza kumemlazimu kuamua ataangazia wapi.
"Kucheza mechi kumi na saba katika wiki saba haiwezekani. Si kamari, ni matokeo tu ya hali ilivyo," alisema.
"Ulikua uamuzi rahisi sana kuufanya, uamuzi wa busara."
Mabingwa wa Europa League huhakikishiwa nafasi katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, sawa na klabu zinazomaliza naafsi nne za kwanza Ligi ya Premia.
Manchester United walishuka hadi nafasi ya sita Jumatano baada ya Arsenal kuwalaza Southampton 2-0 Jumatano.
Arsenal waliwalaza United Jumapili katika mechi ambayo Mourinho aliwapumzisha wachezaji wengi wake nyota kwa ajili ya mechi ya Alhamisi.
Mourinho anaamini kwamba kushinda Europa League ndio njia nzuri zaidi iliyosalia ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Wayne Rooney amefunga mabao saba mechi 38 msimu huu
 Amesema hatakuwa na majuto kamwe iwapo watashindwa kutwaa ubingwa."Hebu tusubiri tuone kama tutaweza," alisema.
"Haijalishi nini kitatokea. Hakuna majuto, tutajitolea kadiri ya uwezo wetu, mimi na wachezaji."
Mshambuliaji wa United Wayne Rooney anaunga mkono msimamo wa Mourinho.
"Kusema kweli, ni vigumu kufuzu kwa kupitia ligi. Tunaweza tukaangazia kushinda kikombe." (BBC)

No comments