MISS TANZANIA AKABIDHIWA GARI LAKE
Mwandishi
wetu
Hatimaye
Miss Tanzania, Diana Lukumay amekabidhiwa zawadi yake ya gari baada ya
kusubiria tangu mwezi Oktoba mwaka jana.
Kampuni
ya Lino International Agency ilishindwa kukabidhi zawadi ya gari kwa
wakati baada ya mdhamini wa kwanza aliyeahidi kutoa zawadi hiyo
kujitoa hatua za mwisho baada ya shindano hilo kuhamia Mwanza.
Hatua
ya kukabidhiwa zawadi mrembo huyo imetokana na agizo la Serikali wa Kampuni ya
Lino International Agency kukabidhi zawadi za warembo walioshiriki katika
mashindano ya mwaka jana ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
Kutokana
na agizo hilo, kampuni ya Lino International Agency ilianza upya juhudi za kutafuta
zawadi kwa mrembo huyo na kuzipata kampuni mbili, kampuni ya uzalishaji na
usambazaji wa vipodozi asilia, Grace Product Ltd na duka la kuuza vito la
Gift Jewellers ambapo kwa pamoja waliamua kununua gari aina ya Suzuki Swift
yenye thamani ya Sh milioni 9.
Mbali
ya kununua zawadi hiyo, kampuni hizo pia zililifanikisha usajili wa gari hiyo
na kupewa namba ya usajiliwa,T625DKL.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Diana amewataka warembo wanaoshiriki
katika mashindano ya Miss Tanzania kuwa wavumilivu ili kukabiliana na
changamoto mbalimbali za mashindano hayo zinazotokana na matatizo ya
kiuchumi.
“Nimefurahi
sana kukabidhiwa gari langu, nimeisubiri kwa muda mrefu na unatakiwa kywa
mvumilivu ili kuendelea kuwa na nidhamu, na sasa kwa kupitia gari langu,
nitafanya kampeni yangu ya kupiga vita mimba za utotoni na unyanyasaji kwa
wanawake kupitia kampuni yake aliyoisajili,” amesema Diana.
Mrembo
huyo pia amewaomba warembo wajitokeza kushiriki katika mashindano ya hayo
pamoja na matatizo yaliyowakumba wao.
“Mashindano
mazuri sana yenye kujenga mtu na kumpatia kipato, tokea nimalize mashindano,
nimeweza kupata dili mbalimbali ambazo sikutaka kuziweka wazi kwenye jamii,
zimekuwa ni shughuli zangu za kila siku,” amesema.
Mkuu
wa Itifaki wa Kampuni ya Lino, Albert Makoye amewashukuru wadhamini wao na kwa
sasa wanaanza pilika pilika za mashindano ya mwaka huu.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Grace Products Ltd, Elizabeth Kilili amesema kuwa,
ameamua kudhamini zawadi ya gari kutokana na kuvutiwa na mashindano na hasa
Diana ambaye anatumia vipodozi vya asili.
Mhasibu
Mkuu wa duka la Gift Jewellers, Faudhia Salum amesema wamemua kuwezesha
zawadi ya gari hiyo, kama moja ya shughuli zao za kijamii.
Salum amesema kuwa
wao kama wauzaji wa vito wamefarijika sana kusaidia mashindano hayo na hasa
ukizingatia kuwa vito vingi uvaliwa na akina dada kwa lengo la kupendeza.
No comments