MECHI ZOTE ZA MWISHO LIGI KUU YA VODACOM BARA
Alfred Lucas Mapunda, msemaji wa TFF |
Mara
baada ya michezo ya mwishoni mwa juma lililopita, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara 2016/2017, inatarajiwa kuendelea Jumanne Mei 9, mwaka huu kwa mchezo mmoja
ambako Mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Young Africans itaikaribisha Kagera
Sugar y Kagera katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia saa 10.00 jioni.
Kwa
mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom, mechi nyingine mbili zitachezwa Ijumaa
Mei 12, 2017 ambako Simba SC itaialika Stand United FC ya Shinyanga kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC siku hiyo hiyo ya Mei 12, mwaka
huu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam ulioko
Chamazi, Dar es Salaam.
Jumamosi
Mei 13, mwaka huu JKT Ruvu itakuwa nyumbani Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
kucheza na Majimaji ya Songea wakati Tanzania Prisons itaikaribisha Ndanda ya
Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga
itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu ulioko Mvomero, Morogoro huku
Mbeya City ikisafiri hadi Dar es Salaam kucheza na Young Africans kwenye Uwanja
wa Uhuru, Dar es Salaam.
Siku
ya Jumapili Mei 14, mwaka huu African Lyon ya Dar es Salaam itacheza na Ruvu
Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali siku inayofuata, Jumanne
Mei 16, mwaka huu Young Africans tena itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Funga
dimba la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakuwa Mei 20, mwaka huu kwa timu
zote kucheza ambako Azam FC itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi,
Dar es Salaam wakati Majimaji itamaliza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Majimaji
mjini Songea wakati Simba na Mwadui zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku
hiyo Mbao FC itaialika Young Africans ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza wakati Stand United itamaliza na Ruvu Shooting ya Pwani kwenye
Uwanja Kambarage mjini Shinyanga ilihali Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Toto
Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro wakati Africans Lyon
ikiwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Ndanda
itamaliza na JKT Ruvu mjini Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
…………………………………………………………………….………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments