Mbunge atoa kilio chake kuhusu soka la Tanzania, aitaka TFF kukuza viwango
Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi |
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi amelitaka shirikisho la soka nchini TFF
kujikita katika kuhakikisha kuwa inakuza viwango timu ya Taifa katika viwango
vya FIFA badala ya kupoteza Muda kwenye vikao vya kuwafungia wadau wa soka.
Akifafanua , Chumi alisema mpaka Machi mwaka huu, Tanzania ilikuwa nafasi ya
157 wakati Taifa kama Afghanistan ambao wako vitani Muda wote walikuwa nafasi
ya 156.
'Ili kupanda katika viwango vya FIFA lazima timu ya Taifa icheze mechi za
kutosha ambazo ziko kwenye kalenda ya Fifa, Sasa kwa mfano mwaka 2016 tumecheza
mechi tatu ukilinganisha na majirani zetu Rwanda mechi 11, Uganda 13, Kenya 10
Afghanistan mechi 6' Alisisitiza Chumi.
Akisisitiza zaidi, Mbunge huyo mwanamichezo alifafanua kuwa katika kipindi
cha miaka mitatu toka 2014-2016 Taifa Stars ilicheza mechi 24 tu kulinganisha
na mechi 47 wakati wa miaka mitatu ya mwisho ya Uongozi wa Leodgar Tenga
2011-2013.
'Ndio mana watu wanamkumbuka Tenga '.
'Ndio mana watu wanamkumbuka Tenga '.
Chumi aliongeza kuwa bila kupandisha viwango vya Fifa, Tanzania itaishia
kuangalia AFCON na Kombe la Dunia kwenye luninga.
'Kupandisha viwango kunasaidia kukwepa kupangwa na timu vigogo, na Ndio mana
kila mwaka tunajikuta katika hatua za awali tu tunapangiwa na Vigogo , mfano
tulipowatoa Malawi tunajikuta tunaangukia kwa Algeria'.
Mbunge huyo alisema kuwa kuthibitisha kuwa kushiriki mechi zilizoko kwenye
Kalenda ya Fifa kunasaidia kupandisha viwango, takwimu zilizotolewa Jana tarehe
4 Mei, 2017 na FIFA , Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 157 mpaka ya 135 baada
ya kucheza na Burundi na Botswana.
Kufungia wadau bila kuwasikiliza sio Sawa , mwaka Jana Kufuatia sakata la
kupanga matokeo ligi daraja la kwanza, baadhi ya wachezaji walifungiwa miaka
kumi.
'Katika soka kumfungia mchezaji miaka kumi ni kummaliza, Hata Ulaya maximum mtu anacheza ni miaka kumi, Sasa unamfungia mchezaji miaka kumi, kweli ndo mana hii ni Tanzania Football Fungiafungia '
'Katika soka kumfungia mchezaji miaka kumi ni kummaliza, Hata Ulaya maximum mtu anacheza ni miaka kumi, Sasa unamfungia mchezaji miaka kumi, kweli ndo mana hii ni Tanzania Football Fungiafungia '
Pamoja na TFF ambayo Chumi aliita ni Tanzania Football Fungiafungia kutokana
na tabia ya hivi karibuni ya kuwafungia wadau wa soka, alivishukia Vilabu vya
soka vya Simba na Yanga kuwa viongozi wake wajitazame haiwezekani mpaka Sasa
havina viwanja.
'Unajiita Rais wa Klabu, je unaacha legacy gani, unajiita Rais wa Yanga,
Rais wa Simba timu inategemea uwanja wa mazoezi wa Boko Veteran, wajitazame.
SOKA LETU SASA LIWE LA KULIPWA.
Akizungumzia soka yetu, Chumi alimtaka Waziri Kuja na mkakati wa kuifanya soka yetu kuwa ya kulipwa Ili Serikali ijipatie mapato.
Akizungumzia soka yetu, Chumi alimtaka Waziri Kuja na mkakati wa kuifanya soka yetu kuwa ya kulipwa Ili Serikali ijipatie mapato.
Soka ni biashara, angalia EPL pamoja na kuwa Timu Yao ya Taifa haiko vizuri
lakini soka yao ni biashara kubwa duniani, michezo ni biashara.
KUTENGA MAENEO YA VIWANJA NA KUVIPIMA.
Aidha Chumi amesisitiza kuwa michezo ni uchumi hivyo lazima Serikali itenge
maeneo ya michezo,
Jukumu hili lazima lihusishe Wizara zote, Tamisemi, Ardhi na ya kwako Mhe Mwakyembe mana peke yako huwezi.
Jukumu hili lazima lihusishe Wizara zote, Tamisemi, Ardhi na ya kwako Mhe Mwakyembe mana peke yako huwezi.
Aliongeza kuwa, kama ilivyokuwa enzi za shule za michepuo ya kilimo,
biashara nk lazima Serikali ianzishe shule za michepuo ya michezo na kukipa
nguvu Chuo cha Michezo cha Malya.
WASANII NA FILAMU ZA NJE.
Chumi alisema kuwa hoja sio kuzuia filamu za Nje bali filamu hizo zilipiwe kodi kama ilivyo kwa Bongo Movie.
'Wasanii wetu wanalipia Cosota, Basata, gharama za ukaguzi Bodi ya Filamu na stika za TRA wakati filamu za Nje hazilipiwi chochote '

Hata hivyo Chumi aliwageukia Wasanii na kuwataka kuifanya kazi ya filamu kwa
weredi Ili kuziwezesha kushindana na kazi za Nje.
Chumi alimalizia kwa kusema kuwa tunaposisitiza michezo kwa sababu ni chanzo
cha mapato na kuongeza kuwa sports and entertainment industry nchini Marekani
inacha
No comments