Header Ads

ad

Breaking News

MANCHESTER UNITED KUKIPIGA FAINALI NA AJAX, SWEDEN MEI 24,2017

United manager Jose Mourinho (left) can't help but laugh as Celta boss Eduardo Berizzo (right) bemoans a missed chance
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho (kushoto), akiangua kicheko, wakati Kocha wa Celta Vigo, Eduardo Berizzo akiziba sura kwa hasira.

Manchester United itashuka uwanjani nchini Sweden kuumana na Ajax ya Uholanzi katika mechi ya fainali ya Kombe la Europa, baada ya usiku wa kuamkia leo kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Celta Vigo ya nchini Hispania bao 1-0.
Katika mchezo huo timu zote zilimaliza pungufu uwanjani baada ya Eric Bailly kwa upande wa United na Rocanglia wa Celta Vigo kuoneshwa kadi nyekundu, wakati mchezo ukielekea ukingoni.
Man United walikata tiketi hiyo kwa bao la dakika ya 17, lililofungwa kwa kichwa na kiugo   Fellaini akitumia vizuri mpira uliopigwa na Marcus Rashford.
Dakika tano katika ya mchezo kumalizika, Celta Vigo walifanikiwa kusawazisha bao hilo lililotumbukizwa wavuni na Sebastian Rocanglia, hata hivyo mfungaji wa bao hilo dakika nne baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu. United imetinga fainali kwa jumla ya mabao 2-1, kwani katika mechi ya kwanza iliibuka na ushindi wa bao 1-0 wakiwa ugenini.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali ya michuano hiyo, Olympique Lyon ya Ufaransa ilitolewa kwenye mbio za ubingwa baada ya kuchapwa jumla ya mabao 5-4. Katika mechi ya kwanza Lyon ilichapwa mabao 4-1  mjini Amsterdam.
Mchezo wa usiku wa kuamkia leo wakiwa nyumbani, Lyon walishinda mabao 3-1, mabao yaliyofungwa na Alexandre Lacazattemabao mawili mbili na Rachid Ghezzal bao moja, wakati bao la wageni lilifungwa na Kasper Dolberg.
Fainali ya michuano ya Europa itapigwa Mei 24, mwaka huu kwenye Uwanja wa Friends Arena jijini Stochklom, Sweden.
Marouane Fellaini (right) celebrates with Jesse Lingard (left) after giving his team the lead in the Europa League clashMarouane Fellaini (kulia), akishangilia na Jesse Lingard, baada ya kuifungia Manchestern United bao katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Europa usiku wa kuamkia leo.
Fellaini (2nd left) is congratulated by his United team-mates after breaking the deadlock at Old Trafford
Fellaini (wa pili kushoto), akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia timu yake bao dhidi ya Celta Vigo kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester, Uingereza usiku wa kuamkia leo.
Roncaglia (centre) races back to the halfway line with his team-mates after equalising in the 85th minute
Roncaglia (katikati), akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake ya Celta Vigo bao dakika ya 85.
John Guidetti shows his dejection after missing a chance to win the tie with the final kick of the game on Thursday
John Guidetti akizikitika baada ya kukosa nafasi ya kucheza fainali ya Kombe la Europa, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester United, lakini imeyaaga mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-1.
French midfielder Paul Pogba (right) breaks away from Namanja Radoja (left) during the first half of the match
Kiungo Mfaransa, Paul Pogba (kulia), wa Man United akimtoka Namanja Radoja wa Celta Vigo katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Europa iliyopigwa Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester, Uingereza usiku wa kumkia leo.

Spanish midfielder Ander Herrera (left) holds off Danish winger Daniel Wass (right) during the semi-final showdownKiungo wa Manchester United, Ander Herrera (kushoto), akiwania mpira, huku winga wa Celta Vigo, Daniel Wass akijadibu kuuwania mpira huo.
United captain Wayne Rooney watches on from the bench after being left out of the starting line-up by MourinhoNahodha wa Manchester United, Wayne Rooney akishuhudia mechi baada ya kuwekwa nje katika kikosi kilichocheza dhidi ya Celta Vigo usiku wa kuamkia leo.
Iago Aspas shows his frustration after having his effort denied by an excellent save from Sergio Romero
Iago Aspas akichukizwa baada ya mpira aliopiga kuokolewa na Sergio Romero
Spanish midfielder Pablo Hernandez (right) unleashes a fierce shot from range which was tipped over by Romero
Kiungo wa Kihispania, Pablo Hernandez (kulia), akimiliki mpira uliopigwa na Romero wa Celta Vigo.

No comments