DC Nyabaganga Talaba awataka Watanzania kupenda kununua bidhaa za ndani
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga
Talaba amewataka Watanzania kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini
ili kwenda sambamba na sera ya Tanzania yenye viwanda pamoja na kuimarisha
uchumi wetu.
Amesema hayo wakati akizindua Baraza la Biashara Wilaya
ambapo alishangazwa na baadhi ya kuamini kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini
hazina ubora na hivyo kukimbilia za nje.
Talaba ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Biashara
Wilaya alisema bidhaa zetu zina ubora kutokana na kutumia malighafi halisi
akitolea mfano viatu vinavyozalishwa na Watanzania ukilinganisha na vinavyotoka
nje ya nchi ambavyo vingi havidumu.
”Tufike mahali sasa tununue bidhaa zetu ili fedha
izunguke kwani tutaimarisha uchumi na kama tunavyofahamu lengo la Rais katika
sera ya nchi ya viwanda anataka tununue bidhaa zetu.
Mkuu huyo wa wilaya alilitaka baraza liwe chachu ya
kusukuma sera ya nchi ya viwanda na kuibua fursa ambazo wananchi waananchi
wanaweza kuzitumia na kuanzisha biashara.
Alilitaka baraza kuja na wazo mbadala la kibishara na kiviwanda
ili wananchi waweze wawaunga mkono wajasirimali wadogo wanaojishughulisha na uzalishaji
wa bidhaa wapate masoko.
Akifungua kikao cha kwanza cha baraza hilo, Mwenyekiti
wa Kamati Tendaji ya Barazaa la Biashara Wilaya, Stephen Magoiga aliwataka
wananchi kutumia vizuri fursa zilizopo wilayani humo.
Magoiga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu alisema tukitumia vizuri rasilimali zilizopo wilayani humo
tutapiga hatua na kujenga historia.
”Tunapozungumzia viwanda siyo lazima viwe vikubwa hata
vidogo vidogo mfano tunaweza kutumia kilimo kuibadilisha kabisa Kishapu na kuwa
wilaya ya kwanza katika uchumi,” alisema.
Alitaja rasilimali kama madini na fursa za kilimo
zilizopo wilayani humo kuwa kama zikitumika ipasavyo maisha ya wananchi yataboreka
zaidi na uchumi kwa ujumla kuimarika.
Baraza hilo la biashara Wilaya ya Kishapu linaundwa na
wajumbe 40 wakiwemo wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi na litadumu kwa
kipindi cha miaka mitatu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la Biashara.
|
Wajumbe wa Baraza la Biashara Wilaya ya Kishapu
wakifuatilia kikao hicho.
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba (kushoto)
akiangalia ngozi ghafi alipotembelea banda la kikundi cha wajasiliamali wa
kutengeneza viatu cha Badimi.
|
Ofisa Biashara Wilaya ya Kishapu, Konisaga Mwafongo
akichangia mada katika kikao hicho.
|
Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa
Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse akizungumza wakati wa kikao.
|
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa
Shinyanga, Jumbe Samson akifafanua jambo wakati wa kikao.
|
Mashine ya kupura nafaka zikiwemo mtama iliyobuniwa na mwananchi wa Kishapu, Daudi Nkende ikiwa katika viwanja vya halmashauri kwa ajili ya maonesho ya wajasiliamali. |
No comments